Nato: Dunia Yote Inastahili Kuichukulia Hatua Korea Kaskazini
0
September 11, 2017
Katibu mkuu wa shirika la kujihami la nchi za magharibi Nato Jens Stoltenberg, amesema kuwa mpango wa nyuklia wa korea Kaskazini na tisho kwa dunia nzima.
Lakini hata hivyo alikaa kusema ikiwa shambulizi kwenye himaya ya Marekani ya Guam linaeza kusababisha hatua za pamoja za kijeshi.
Kipengee cha tano cha makubaliano ya Nato kinasema kuwa shambulizi dhidi ya mwanachama mmoja ni shambulizi dhidi ya wanachama wote.
Guam ambacho ni kisiwa himaya ya Marekani kilicho bahari ya Pacific ni kituo muhimu cha kijeshi na kimetishiwa mara kwa mara na Korea Kaskazini.
Korea Kaskazini yasifia jaribio jingine la nyuklia
Korea Kusini yafanya majaribio ya makombora kujibu majaribio ya Korea Kaskazini
"Siwezi kusema ikiwa kipengee cha tano kitatumiwa wakati wa hali kama hiyo," Bw Stoltenberg alisema.
Alitoa wito wa Korea Kaskazini kuacha kuunda zana za nyuklia akisema kuwa huo ni ukiukaji mkubwa wa maazimio ya Umoja wa Mataifa,na tisho kwa amani ya dunia.
Matamshi ya Bw Stoletnberg yanakuja wakati wanachama wa baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa wanatofautiana kuhusu njia za kuukabili mzozo wa Korea Kaskazini kufuatia hatua yake ya hivi punde ya kufanyia jaribio kombora kupitia anga ya Japan.
Tags