Natumia Mitandao ya Kijamii Kutoa Habari Zangu Mara kwa Mara Ila Sitengenezi Kiki- Diamond

Natumia Mitandao ya Kijamii Kutoa Habari Zangu Mara kwa Mara Ila Sitengenezi Kiki- Diamond
Msanii wa Bongo Flava, Diamond Platnumz amekana suala la kutengeneza kiki katika mitandao ya kijamii.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Love You Dia’ aliyoshirikishwa na Patoranking, ameiambia Radio Maisha, Kenya kuwa mitandao yake anaitumia kuwajuza mashabiki taarifa mbali mbali na sii vinginevyo.

“Hamna, mimi kama kwa mfano kwenye Instagram na kwenye mitandao yangu ya kijamii nawapa habari zangu zinazotokea mara kwa mara. Kazi yangu mimi ni ya muziki, kwa hiyo watu wanakuwa wanaburudika,” amesema Diamond.

“Huwa naweka mwenyewe, wapo digital management pale ofisini kwetu lakini ile niwe active sometimes huwa nafanya mwenyewe,” ameongeza.

Diamond katika mtandao wa instgrama ana followers 3.9 milioni, twitter 429k facebook like 2. milioni.



Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na anavyowaita watu bitch. huwa hatafuti kiki.

    ReplyDelete
  2. wacha uongo kiki unaipenda na ukiona ziii basi unatuletea ajuza wako hio inaitwa nini? let me advise you wacha mbwe mbwe nyingi hupendezi ukitaka kuanza kutikana watu na kujigamba na utajari k7mbuka ulipo toka usije ukapata pigo ukarudi chini siseme hukukanywa wacha kutukana dada za watu na kuwaharibia wenzako kazi zao kubali kushindwa nduo uungwana

    ReplyDelete
  3. Domo mnafiki sana. anajifanya mtu mweama sana wakati anawaaribia wenzie, akiona hana kiki anaitafuta mpaka kwa ajuza wake.ila akumbuke alie juu mngoje chini.

    ReplyDelete
    Replies
    1. wote mliochangia hapo juu ni vilaza hamjitambui wala kujielewa

      Delete
  4. I think wewe ndio big kilaza including huyu unae side na yeye unaitafuta kiki kwa nguvu true na kama hupati anamtumia ajuza wake haaaaaaaa eti ajuza lakini jamani ni ajuza just look at her hands from top oh OMG ni ajuza anyway so usijibabaishe kusema you aren't looking for kiki mhh mhh no

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad