Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, amesema anaungana na Rais Magufuli, viongozi wengine na wananchi, katika kumuombea Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu aliyepigwa risasi.
Akisoma hotuba ya kughailisha bunge mapema leo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema anamuombea Tundu Lissu ili aweze kupona na kurejea katika hali yake ya kawaida na kwenye shughuli zake kwa jamii.
“Naungana na Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Mheshimiwa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Spika wa Bunge Job Ndugai, wabunge na wananchi mbali mbali, kumpa pole kwa majeraha na maumivu makubwa anayoyapata, na tunamuombea apone haraka na kurejea kwa familia yake, lakini pia na sisi hapa bungeni kwa shughuli za bunge”, amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Leo waziri mkuu ameghailisha shuguli za bunge kwa mujibu wa sheria, mpaka hapo Novemba 7 mwaka 2017 litakapoanza vikao vyake tena
Naungana na Mh.Rais, Viongozi Wengine na Wananchi Katika Kumuombe Tundu Lissu- Waziri Mjaliwa
1
September 15, 2017
Tags
Ameen.....!!!!!!
ReplyDeleteSwadakta.. Mh Kassim Majaliwa.
Swadakta.. Baba JPJM
Swakta Mh Mipango.
Nnnasema Dodoma ni Tulivu na Ina Pumzisha vichwa na Fikra.. Maamuzi na Maagizo yake ni Mazito.
Mnakaribishwa sana Dodoma na Tuendelee kuifanyia kazi nchi yetu kutokea Dodoma.. Ninayo imani Tanzania yetu mpya is achievable in even shorter than expected time.
Miongozo toka Dodoma na Ufatiliaji ni Nchi nzima.
Napendekeza tuunde wizara ya Ufatiliaji ambayo itakuwa haina kikomo katika utendaji na ufatiliaji
ambayo itakuwa chini ya Ofisi ya Waziri mkuu. Mimi Nikiwa ni waziri wake itakuwa na sifa ya kiutendaji na bajeti yake. and board members wake ni manibu waziri wa kila wizara teule.
Hii itasaidia uendeshaji na urahisishaji wa maamuzi ya Nchi. na kunsaidia Baba yetu JPOJM katika ufatiliziaji na utekelezaji ambao pia unakuwa katika meza ya Ofisi ya Waziri Mkuu. ( Hii ni pendekezo) Linahitaji kufikiriwa na Decisiom makers .
Tanzania Kwanza na Uzalendo Mbele.
Hapa Kazi Tu.