Ndugai Atoa Ufafanuzi wa Adhabu Anazozitoa Bungeni

Ndugai Atoa Ufafanuzi wa Adhabu Anazozitoa Bungeni
Spika wa Bunge la Tanzania, Mh. Job Ndugai  amefafanua kauli yake ya kuhusu adhabu ambazo huwa anazitoa bungeni ikiwepo kauli ya kutaka kumzuia Zitto kuzungumza bungeni na kusema hizo huwa ni adhabu za Spika kutokana na dharau ambazo zinaonyeshwa.

Akizungumza hivi karibuni na East Africa Radio Mh. Ndugai amesema kwamba ingawa huwa kuna adhabu ambazo hutolewa na kamati ya Maadili lakini yeye kama Spika huwa ana adhabu ambazo analazimika kuzitoa kwa kuwa ana mamlaka ndani ya bunge na ndiyo mwenye nafasi ya kutoa au kuzuia ruhusa wakati wa uchangiaji bungeni.

"Zipo adhabu za Kamati ya Maadili ambazo hutolewa lakini pia Spika ndani ya bunge anauwezo na mamlaka ya kutoa nafasi ya kuongea ndiyo maana hata wakati wa kuongea sentensi ya kwanza huwa wanasema Mh. Spika sasa anapotokea mtu ambaye anakudharau na anakutukana hadharani bila sababu kwa nini umpatie nafasi ya kuzungumza mtu huyo? amekuwa shangazi yako? Ni suala la kuheshimiana tu. Kama humuheshimu mtu kwa nini wewe uheshimiwe? Ndugai

Spika Ndugai ameongeza kwamba  " Mara nyingi Wabunge ambao huwa wanaofanya vitendo hivyo ni wale ambao wameshaingia bungeni hata mara ya nne lakini utamkuta anamdhalilisha Spika bila sababu na hata akipelekwa kwenye kamati ya maadili akihojiwa na Wabunge wenzake utakuta hana sababu maalumu ya kutoa"
Msikilize Spika Ndugai hapa chini akifafanua wakati akifanya mahojiano na kipind cha East Africa Breakfast

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad