Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Kombwey ametangaza kumteua Mbunge ndugu Rehema Juma Migira kuwa Mbunge wa viti maalum kupitia Chama Cha (CUF) kufuatia kifo cha mbunge mteule Bi Hindu Mwenda aliyefariki dunia Septemba 1, 2017.
Kailima amesema Tume ya Uchaguzi imefanya uteuzi huo baada ya kupata taarifa kutoka wa spika wa bunge, Job Ndugai kuwepo kwa nafasi moja ya ubunge kufutia kifo cha mbunge huyo mteule ambaye alifariki siku tatu kabla ya kuapishwa.
"Tume ya taifa ya uchaguzi imemteua ndugu Rehema Juma Migira kuwa mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupata taarifa kutoka wa spika ambaye alitutaarifu kuwepo kwa nafasi moja ya wazi ya viti maalumu kupitia chama cha CUF baada ya aliyeteuliwa kuwa mbunge wa viti maalum CUF kufariki dunia" alisema Kailima
Aidha Kailima aliendelea kusema kuwa tume hiyo imefanya uteuzi pia wa madiwani wa viti maalum watatu kujaza nafasi wazi katika halimashauri za Tanzania bara madiwani hao ni pamoja na ndugu Jane Chungwa kutoka CCM ambaye anakuwa diwani wa viti maalum halmshauri ya Itigi Singida, Ndugu Osana Mwinyi kutoka chama cha CCM anakuwa diwani wa viti maalum halmshauri ya Bahi Dodoma na ndugu Pili Mfaume kutoka chama cha CUF anakuwa diwani wa viti maalum halmshauri ya Temeke, uteuzi huo wa madiwani umefanyika baada ya tume kupata taarifa ya kuwepo kwa nafasi hizo wazi kutoka kwa waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa.