Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt John Pombe Magufuli amesema ameona shida ya Ikulu na kwamba ni mateso kuwa Rais wa chi na yeye amekiri kuwa ameshuhudia mateso hayo japo aliomba nafasi hiyo ya uongozi kwa kujaribu.
Akiwa mkoani Arusha baada ya akiwatunukia Kamisheni Maafisa wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Rais magufuli amesema kwamba aliomba nafasi hiyo kuongoza kwa kujaribu lakini mwishowe akasukumiziwa na sasa anaona mateso yake hivyo hana budi kutatua shida za watanzania.
"Naifahamu hii kazi nayoifanya ni ngumu, ni msalaba inahitaji kumtanguliza Mungu kweli kweli . Kwa sababu ni kujitoa sadaka lakini nimekubali kuwa sadaka kwa ajili ya watanzaniakwa ajili ya kuwanyoosha mafisadi waliozoea kuwaibia watanzania" amesema
"Ninaamini inawezekana hapatatokea mwingine ambaye atajitoa hivi. Najua siku moja mtakumbuka Hamju mateso ninayoyapata. Ni shida kuwa Rais. ndi maana Baba wa Taifa aliwahi kyusema pale Ikulu ni mateso. Mimi nimeyaona mateso niliomba kwa kujaribu wakanisukumizia huko. Magufuli
Amesema kwa kuwa watanzania wamempa nadfasi ya kuongoza basi atawatumikia kwa uaminifu kwani hakutoa Rushwa wala kuchangiwa hela na mafisadi kuingia ikulu ndiyo maana haogopi kutumbua na kuwahakikishia wananchi kwamba atazidi kutumbua kweli kweli
Pamoja na hayo amewatakaa wananchi waachane na mambo ya vyama kwani hayana faida kama watakuwa na njaa
Ungejaribu kufata sheria za nchi na katiba, pamoja na heshima kwa wananchi wako,labda yangekuwa nafuu,lakini kujifanya ubabe usio na tija, ndio lawama na matusi unayoambulia kila dakika.
ReplyDeleteMbona povu linakutoka......ni wewe au baba'ko katumbuliwa?? Pole yako, HAPA KAZI TU!
Delete