Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amefunguka na kudai amesikitishwa na kitendo cha Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwataka wabunge wawili kufika mbele ya Kamati ya Maadili na mwengine kamati ya ulinzi na usalama kuhojiwa juu ya kauli zao walizozitoa
Mhe. Godbless Lema amesema hayo leo akiwa mjini Nairobi nchini Kenya alipokwenda kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye ameshambuliwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
"Nimesikitishwa sana na kitendo cha Mhe. Spika kuwataka wabunge wawili, Mhe. Zitto Kabwe na Saed Kubenea kutokea katika kamati ya maadili na mwingine kamati ya ulinzi na usalama na pengine baada ya maneno yangu haya na mimi naweza nikaitwa lakini siyo kitisho tena kwangu kuitwa mahali popote. Nipo Nairobi kumuangalia mbunge wetu na rafiki yangu, Mhe. Lissu ambaye hawezi kula wala kuinua mkono baada ya kupigwa na risasi na watu wasiojulikana", amesema Lema.
Pamoja na hayo, Lema ameendelea kwa kusema "Nilitarajia Mhe. Spika aliposikia taarifa za mbunge wake kupigwa risasi pengine shughuli za Bunge zote angesimamisha kama ambavyo alivyoamuru kukamatwa kwa wabunge wawili wapelekwe Polisi akiwemo Kubenea hapo awali", amesisitiza Lema.
Kwa upande mwingine, Mhe. Godbless Lema amedai alitarajia kuona mabadiliko ya katika Bunge kwa kupitisha sheria kwa pamoja ili kusudi wabunge waweze kupatiwa ulinzi wa kutosha kuanzia majumbani kwao mpaka wao wenyewe lakini imekuwa tofauti na yeye alivyokuwa akifikiri.
Fuata process kama wengine TL ni Mtanzania kama wengine Maamuzi ya kwenda nje ni lazima yatolewe Muhimbili. CDM mnataka shortcut. Is sad kwa TL lakini process is process.
ReplyDeleteprocess gani unayoizungumzia hiyo, wacha upumbavu wako jiongeze kama ujenda shule, use your common sense, au wewe ndio wale wale kama Spika, anafata matakwa ya mshenzi mweziwe. kuwa mzalenda. usiwe na chuki na vizasi vya kulionesha kama magufuli.
ReplyDeleteUkitoa hoja kwa kutumia lugha ya kawaida hautasikika?
DeleteSPIKA NI MPUMBAVU TU HANA HIKMA WALA BUSARA, HATUFAI MAKUFULI AFANYE MPANGO KUMPELEKA INDIA AKATIBIWE TENA ,THIS TIME MENTAL ILLINESS.
ReplyDeleteMbona mnachanganya mada hapa.
ReplyDeleteWewe godless unasema nini.
Ya Mh Raisi yameingiaje hapa.
ya Mh Job NDUNAI YAMEKUJAJE HAPA.
TL anauguzwa ..ni mmoja kama mwananchi mwingine yeyote.
cha zaidi kwake ni kipi.
MUWACHAGE KUTUCHANGANYAGA
MLIO CHANGANYIKIWAGA.
kuna idadi gani ya wabunge Tanzania? Je, inaleta mantiki kwa kila mbunge apatiwe ulinzi majumbani na wakati wowote?Na nani atagharamia huduma hiyo?
ReplyDelete