Nissan Yaja na Ujio Mpya wa Magari Yanayotumia Umeme

Nissan Yaja na Ujio Mpya wa Magari Yanayotumia Umeme
Kampuni ya magari ya Nissan imezindua magari mapya ya umeme, wakati inakabiliana na ushindani unaozidi kukua wa magari ya umeme
Aina hiyo mpya ya magari yanaweza kusafiri mwendo wa asilimia 50 zaidi baada ya kupata chaji, kwa mujibu wa kampuni hiyo.

Hata hivyo bado magari hayo hayajafikia mwendo wa magari wa Tesla na GM.
Magari hayo yanayofahamika kama 'Leaf' yanakabiliwa na ushindani mkali wakati sekta ya magari yanayotumia umeme inazidi kukua.
Magari mapya ya Leaf yameuzwa nchini Japan kuanzia Oktoba na yataanza kuuzwa sehemu zingine mwaka ujao.

Kati ya mabadiliko yaliyofanyiwa hayo magari hayo ni mfumo wa kujindesha unaofahamika kama ProPilot Park, ambao huyawezesha kepenya maeneoimagumu hususan wakati wa kuegeshwa.
Pia yana teknolojia ya kujiendesha yenyewe hasa kwenye babara ambayo inaelekea upande mmoja tu.
Bei ya magari hayo itaanzia yen 3,150,360 au pauni 22,220.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad