Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis jana Ijumaa ameongoza tendo la upatanisho kati ya wapiganaji wa zamani na waathirika wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Kolombia, akiomba "ukweli" na "haki" kwa waathirika wa vita hivyo vya nusu karne.
Raia waliojeruhiwa na waliopoteza wapendwa wao na wapiganaji wa zamani walibadilishana maneno ya msamaha na kulia huku Papa Francis akihimiza nchi kuondokana na mgogoro huo mrefu zaidi katika nchi hiyo ya Amerika Kusini
Akiwa katika mji mkuu wa Villavicencio Papa Francis amesema katika mchakato huu wa muda mrefu, mgumu, lakini wa matumaini ya upatanisho, ni muhimu kuzingatia ukweli.
Papa Francis ameongeza kuwa ukweli ni rafiki asiyeweza kutenganishwa na haki na huruma na vyote kwa pamoja ni muhimu katika kujenga amani.
Papa Afanya Usuluisho na Upatanishi Nchini Colombia na Kuomba Ukweli na Haki
0
September 09, 2017
Tags