Polepole ameeleza hayo kupitia ukurasa wake maalumu wa facebook mchana wa leo huku akinukuu baadhi maneno aliyowahi kuyatoa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambayo yalikuwa wazi kabisa yakiongelea namna ya kujikomboa ili bara la Afrika kiujumla liweze kufikia uhuru wake wa kiuchumi.
"Leo Afrika nzima inazizima kwamba yuko mwanaume ambaye ameweza kusema imetosha 'enough is enough' siyo haki na ni unyonyaji kuchukua madini yetu katika namna ambayo haki yetu inapokwa. Ndugu Magufuli ana amini sana katika sekta binafsi na hasa katika ujenzi wa uchumi wa viwanda sambamba na sekta ya umma. Lakini ana amini zaidi katika sekta binafsi inayojiendesha kwa kanuni za maadili ikiwemo kulipa kodi. Anaamini katika uwekezaji kutoka nje, lakini unaotambua kwamba sisi ni taifa huru na tunayo haki ya kunufaika kutokana na utajiri wa rasilimali zetu", ameandika Polepole.
Aidha, Polepole amesema CCM imemleta Rais Magufuli katika wakati muafaka ambapo nchi ilikuwa inaelekea pabaya.
"Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemleta ndugu Magufuli wakati muafaka wakati tunamuhitaji zaidi mtu kama yeye. Ukisoma maelezo na nukuu za Mwalimu Nyerere katika maelezo yangu ya awali juu ya maono ya Mwalimu Nyerere utaungana nami kusema ile aina ya uongozi mpya katika bara la Afrika, Tanzania tumekuwa kinara wa kwanza na wengine watafuata ili bara la Afrika lirejeshe heshima yake ya uhalisia na asili", amesisitiza Polepole.
Kwa upande mwingine, Polepole amesema ipo siku ataeleza ni kwanini Rais Magufuli amekuwa zawadi katika taifa la Tanzania kwenye kipindi hiki.
Acha Upotoshaji polepole. Mtu mmoja hazimishi bali kundi la watu. Acha siasa za ukandamizaji wa kisiasa na kumtukuza mtu mmoja au kumpa hadhi ya waliofungawa midomo.Unatumia chama kumtukuza kiongozi mkuu wa serikali akisahau yeye ni kiongozi wa nnci na serikali nzima. Unapotosha umma kwa kusema CCM ndiyo bila haya ukijua wazi CCM isingeibia nchi, isingesaini mikataba mibovu, isingetetea PTL, ESCROW leo Tanzania ingekuwa mbali sana. Mnaziba ukwkweli kutunukia uovu, kama hakuna elimu nchini.Wenye elimu wanajua ingawa mnawaogopesha. Hakuna mtu hata mmoja nchini asiyejua kwamba ni CCM chini ya viongozi hawawa kwa miaka kumi na tano, mmewaziba midomo kila Mtanzania anayejaribu kufichua mbinu zunu ambazo ni toka siku nyingi zimetendeka nabaadhi ya wanachama, udhaifu wenu kichama, ufisadi wa baaddhi ya wanachama na mambo makubwa yote ambayo yanafichwa, yatafichuka tu.Kunawatu ndani ya CCM ni wasafi na hawapo tayari kuona Taifa likitikisika kwa kuwaficha waovu kisa Chama. Sidhani.Naamini wengi Wanachama ndani ya CCM ambao hawana hatia na hodari iku siku watasema ukweli. Naamini.
ReplyDelete