Polisi Kuchunguza Shambulio la Risasi Alilofanyiwa Tundu Lissu

Polisi Kuchunguza Shambulio la Risasi Alilofanyiwa Tundu Lissu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amezungumzia tukio la kupigwa risasi mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, akiwaomba wananchi wenye taarifa kulisaidia jeshi hilo.

Muroto amesema leo Alhamisi kuwa wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na wameshafika eneo la tukio nyumbani kwa Lissu.

“Tunaomba mwananchi wenye taarifa atusaidie. Jeshi la Polisi tumeanza uchunguzi, tumefika eneo la tukio na tunaendelea,” amesema.

Kamanda Muroto amesema taarifa za awali zinaonyesha kuna gari aina ya Nissan lenye rangi nyeupe lilikuwa likimfuatilia Lissu.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana amewataka wananchi kuwa watulivu wakisubiri taarifa za Jeshi la Polisi na madaktari wanaoendelea na matibabu ya mbunge huyo, ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa Chadema.

Akizungumza maendeleo ya matibabu ya mwanasiasa huyo ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma James Charles amesema Lissu yu hai na imara.

Amsema mbunge huyo amepigwa risasi tumboni na kwamba timu ya madaktari inaendelea na matibabu.

“Tumempokea Lissu mchana, kanuni za matibabu haziruhusu mtu mwingine asiye mtumishi kuingia chumba cha matibabu. Tuna uwezo wa kutosha wa kutoa huduma ya dharura,” amsema.

Amsema kwa sasa wanaendelea na huduma na wakikamilisha watatoa taarifa.


Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. watachunguza nini na wanajua nani alowatuma kumuuwa Lisu? msijishaue watanzania wanajua kila kitu.

    ReplyDelete
  2. Well say wanafunga Banda wakati farasi keshatoka mumempiga wenyewe halafu munafanya uchunguzi imekua paka Wa mfalme lkn uko siku mfalme utaliwa na paka wako

    ReplyDelete
  3. WA kwanza katika usaidizi.
    Waliotueleza hili yendo ni mlolongo wa uongozi wa Bawicha.
    Hili linajulikana .
    Struggles within inner circles of party powers.
    Mwenyekiti / Katibu/ Mweka jazina/ mwanaselia( sasa viktom) wote hawa Kula mmoja Ana mwelekeo WA kuona mwenzake anatokewa .sasa nani anamwanza hapo itabidi serikali na vyombo vya dola vipate muono.
    Kuwakosea Watanzania Ni kiss lisilo na msamaha.
    Tutakielewa kinacho endelea na bawicha watajieleza nano anajua nini.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad