Polisi Kuzuia Maombi Ya Lissu Haitoathiri Afya Yake Ila Waliotangulia Mbele za Haki Wanamuombea Moja kwa Moja- Sugu

Polisi Kuzuia Maombi Ya Lissu Haitoathiri Afya Yake Ila Waliotangulia Mbele za Haki Wanamuombea Moja kwa Moja- Sugu
Mbunge  Joseph Mbilinyi, ‘Sugu’ amedai marufuku ya jeshi la Polisi kuzuia  maombi maalum kwa ajili ya Tundu Lissu haitaathiri afya yake kwani yeye anaamini viongozi na wanachama wa chama waliotangulia mbele za haki wanamuombea moja kwa moja kwa Mungu

Sugu aliyasema hayo  wakati wa Ibada ya mazishi ya aliyekuwa Diwani wa viti Maalum kupitia (CHADEMA) jiji la Mbeya Esther Mpwiniza aliyefariki dunia ghafla Septemba 16, mwaka huu kutokana na Shinikizo la damu.

Sugu alisema kwa kuwa jeshi la polisi limezuia ibada kwa ajili ya kumuombea Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu aliyejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana yeye anaamini wanachama waliotangulia mbele za haki watafanya kazi hiyo kwa niaba ya wanachama.

Sugu aliendelea kusisitiza kuwa mbali na kupiga marufuku kufanya maombi pia serikali imekuwa ikiwazuia watu kwenda kwenye misiba ambapo alidai viongozi na wanachama walizuiwa kuhudhuria msiba wa aliyekuwa mbunge wa Moshi Mjini Marehemu, Philemon Ndesamburo.

“Naamini Kamanda wetu Esther saizi upo moja kwa moja na Malaika naomba ukamuombee Tundu Lissu apone haraka anyanyuke kutoka kitandani aendelee na kazi za ukombozi wa taifa letu, huku wametuzuia kufanya maombi lakini huko najua hawezi kufika kuwazuia,”alisema Sugu

Akizumzungumzia marehemu Mpwiniza Sugu alisema alikuwa ni mwalimu wa siasa na mpiganaji wa kweli kwa ajili ya maslahi ya wananchi wa jiji la Mbeya pamoja na chama na kwamba mchango wake umefanikisha ushindi wake kwa kiwango kikubwa. Amedai marehemu alikuwa ni ngao na mtu mwenye tabia ya kuwaunganisha wanachama na kuondoa tofauti ambazo zililkua zinatoa mwanya wa kuwepo kwa makundi ndani ya chama hicho.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad