Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto |
Pia Kamanda huyo alimtaka Katibu Mkuu wa Chadema Dk Vicent Mashinji kufika kwa RCO mjini Dar es Salaam ama Dodoma kutokana kauli yake kuwa katika uchunguzi wao wamewabaini wahusika.
Kamanda Muroto amesema Polisi Mkoani Dodoma wamekamata magari nane aina ya Nissan Patrol kwa ajili ya uchunguzi wa tukio la kupigwa kwa risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema)Tundu Lissu.
Kamanda Muroto amesema uchunguzi huo unafanywa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA).
"Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa wahalifu walikuwa na silaha ya SMG/SAR kutokana na maganda ya risasi yaliyokutwa eneo," amesema
MY TAKE
Polisi waanze na Walinzi/Polisi wa mageti yanayoingia kwa Lissu. Huwezi pita kwenye geti linaloenda kwenye makazi ya Viongozi bila Kibali. Na nyumba ya Lissu ipo jirani na nyumba ya Spika. Je wale maaskari hawajasikia Milio ya Risasi 32?
Kwanini waliwafungulia wahalifu hata baada ya tukio?
Tuanze na Askari wa zamu nyumba za Viongozi wa pale getini.
Camera inaonesha gari lililopita ni plate namba gani? Tupeni namba tuanze kuisaka, kusema gari nyeupe tu haitoshi, magari meupe mengi.
Swali zyri hilo. Je wamehojiwa? Je Haya magari mawili hayakupita hapo. Kama yalipita basi wameliona. Je hawana kamera? Je hakuna kituo Dodoma kuelekea huko chenye kamera?
ReplyDelete