Putin: Vikwazo Dhidi ya Korea Kaskazini ni Bure

Putin: Vikwazo Dhidi ya Korea Kaskazini ni Bure
Rais wa urusi Vladimir Putin amesema kuwa vikwazo zaidi dhidi ya Korea Kaskazini ni bure, akiongeza ni radhi wale nyasi kuliko kuachana na mpango wao wa nyuklia.
Marekani ilisema Jumatatu kuwa itapeleka azimio mpya kwa Umoja wa Mataifa la vikwazo zaidi, kufuatia hatua ya nchi hiyo kulifanyia majaribio bomu la nyuklia siku ya Jumapili.
Bwana Putin pia alisema kuwa hatua za kijeshi inaweza kuleta janga la dunia nzima.

Amesema kuwa mazungumzo ndiyo njia pekee.
China, mshirika mkuu wa Korea Kaskazini pia nayo imetaka kurejelewa kwa mazungumzo.

Putin alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa nchi za Brics ambazo ni (Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini) huko Xiamen nchini China.
Licha ya Putin kuishutumu Korea Kaskazini, alisema kuwa vikwazo havitasaidia.

Siku ya Jumatatu mjumbe wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley, alisema kuwa vikwazo vikali vitasababisha tatizo hilo kutatuliwa kwa njia ya kidiplomasia.
Chansela wa Ujerumani Angela Merkel aliunga mkono pendekezo hilo akisema kuwa vikwazo vya haraka vinahitajika kukabiliana na tabia ya Korea Kaskazini kukiuka maazimio ya kimataifa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad