Rais John Magufuli Aungana na Wasabato na Kuchangisha Mil 25.3 za Ujenzi wa Kanisa


Rais John Magufuli  ameungana na waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato katika ibada ya sabato iliyofanyika Usharika wa Magomeni Mwembechai na kuchangisha zaidi ya Sh25.3 milioni kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo.

Rais Magufuli akiwa na Mkewe Janeth Magufuli  katika ibada hiyo iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo,  alisema  Serikali itaendelea  kushirikiana na viongozi wa dini katika kuwahudumia wananchi.

Rais Magufuli amewahakikishia waumini na viongozi wake kuwa Serikali inatambua mchango huo na itaendelea kushirikiana na madhehebu yote ya dini katika kuwahudumia wananchi.

“Baba Askofu na kushukuru  kwa mahubiri mazuri ya leo ambayo yamenigusa , madhehebu ya dini likiwemo hili la Waadventista Wasabato mnatoa mchango mkubwa sana kwa Taifa letu, nakuhakikishia kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nanyi” amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alitoa mchango wa Sh5 milioni ya ununuzi wa mifuko 400 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa jipya la Waadventista Wasabato kwenye eneo hilo na Sh1 milioni kwa ajili ya kwaya za Kanisa hilo.

Katika ibada hiyo iliyohudhuriwa na maaskofu wengine akiwamo Askofu wa Jimbo la Mashariki Kati, Joseph Mgwabi na Askofu wa Jimbo la Kusini Mashariki, Albert Nziku, Rais Magufuli aliendesha  harambee ya papo kwa papo ya kuchangia ujenzi wa Kanisa, na kufanikisha kupata  25.3 milioni.

Katika salamu zake,  Askofu Malekana alimshukuru Rais Magufuli kwa kuungana na waumini wa Kanisa hilo katika Ibada ya Sabato na kuchangia ujenzi wa kanisa, na ameongoza maombi ya kuliombea Taifa na Rais.

By Mwananchi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad