Rais Magufuli Ameagiza Madini ya Tanzanite Kuwekewa Ulinzi na Jeshi

Rais Magufuli Ameagiza  Madini ya Tanzanite Kuwekewa Ulinzi NA Jeshi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza Jeshi la Wananchi kushirikiana na Suma JKT kujenga ukuta mkubwa kuzunguka eneo lenye madini ya Tanzanite na kuweka mitambo maalum, ili kulinda madini hayo yasiendelee kuibiwa.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wilayani Simanjiro Mkoani Manyara ambako ameende kuzindua barabara ya lami iliyojengwa kwa bilioni 32.5 ya KIA- Manyara, na kusema kwamba ni lazima ulinzi huo uwekwe ili kuokoa rasilimali za Tanzania zisiendelee kuibiwa na nchi kubaki masikini.

"Eneo la Simanjiro kuanzia Block A mpaka Bolock D ambalo lina madini mengi, ninaagiza Jeshi la wananchi likishirikiana na Suma JKT, waanze kulijengea ukuta eneo lote, wataweka fensi juu na wataweka camera, patawekwa mlango mmoja na itawekwa mitambo maalum, hata kama utameza Tanzanite itaonekana, hata ukificha kwenye kiatu itaonekana", amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli atakuwepo mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku 3, ambapo pia atatoa kamisheni kwa maafisa waliohitimu mafunzo ya jeshi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Septemba 23, 2017.

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sawa Sawa Baba...!! Tumeibiwa sana Mkuu... Tafadhali piga full stop.
    Tanzania si nchi ya kuomba... Ni tajiri.
    Sisi si wakukosa Dawa Hospitali and kuona kina mama wanafia katika Uzazi na mengine mengi.
    Mungu akuweke utunyooshee nchi yetu and wanaopewa Dhamana za usimamiaji ni lazima wawe Waadulifu.

    ReplyDelete
  2. Well done magufuli

    ReplyDelete
  3. Haitosaidia kitu chochote wasting money and time for nothing ukweli ni kuwa wizi utaendelea tu kama kawa no matter what mbongo ameishazoea kuishi kwa kupiga dili humwambii kitu ukiziba hapa yeye anafukua kule anaendeleza libeneke kazi hakuna na hata hizo chache mtu akipata nafasi ya kufanya kazi mshahara wenyewe mbuzi sasa unafikiri mbongo atakuelewa?Wewe ni jeshi la one man army against millions of Tanzanians who are poor

    ReplyDelete
  4. Haitosaidia kitu chochote wasting money and time for nothing ukweli ni kuwa wizi utaendelea tu kama kawa no matter what mbongo ameishazoea kuishi kwa kupiga dili humwambii kitu ukiziba hapa yeye anafukua kule anaendeleza libeneke kazi hakuna na hata hizo chache mtu akipata nafasi ya kufanya kazi mshahara wenyewe mbuzi sasa unafikiri mbongo atakuelewa?Wewe ni jeshi la one man army against millions of Tanzanians who are poor

    ReplyDelete
  5. Haitosaidia kitu chochote wasting money and time for nothing ukweli ni kuwa wizi utaendelea tu kama kawa no matter what mbongo ameishazoea kuishi kwa kupiga dili humwambii kitu ukiziba hapa yeye anafukua kule anaendeleza libeneke kazi hakuna na hata hizo chache mtu akipata nafasi ya kufanya kazi mshahara wenyewe mbuzi sasa unafikiri mbongo atakuelewa?Wewe ni jeshi la one man army against millions of Tanzanians who are poor

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad