Rais John Magufuli anatarajiwa kuwasili mkoani Arusha kesho kwa ziara ya siku tatu.
Akitoa taarifa hiyo ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, amesema baada ya kuwasili, anatarajiwa kuzindua barabara ya KIA Mererani inayoanzia Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro hadi mji wa Mererani mkoani Manyara.
Kwa mujibu wa Gambo Septemba 23, Rais Magufuli anatarajiwa kutunuku kamisheni kwa maafisa wa jeshi, tukio litakalofanyika katika uwanja wa Shekh Amry Abedi jijini Arusha.
Pia amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuhudhuria sherehe hizo.
Sherehe hizo ambazo kwa kawaida hufanyika katika chuo cha maafisa wa jeshi cha TMA, zinafanyika kwa mara ya kwanza katika uwanja huo jambo ambalo linatoa fursa kwa wananchi wa Arusha kushuhudia
Rais Magufuli Kuanza Ziara ya Siku Tatu Mkoani Arusha Kesho
2
September 19, 2017
Tags
Si mikusanyiko ya hadhara imezuiliwa? vipi sasa. Kuna exceptional. Kwani si sheria moja kwa wote. Mikutano ya siasa imepugwa marufuku.
ReplyDeleteTumia akiri we so unataka akae tu! Huyo ni rais Wa nchi tofauti na wabunge wanaomiliki majimbo tu! Kumbuka wabunge hawajakatazwa mikutano ktk majimbo yao Bali wamekatazwa nje ya majimbo yao! Nikuulize je rais afanye mikutano ktk jumbo gan? Je akae tu bila kutembelea wananchi wale,? Maana ya kuwa rais n ipi?
Delete