Rais Dk. John Pombe Magufuli leo atapokea taarifa ya uchunguzi wa madini ya Tanzanite na Almasi uliofanywa na kamati maalum mbili zilizoundwa na spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.. Job Ndugai.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa , amesema, taarifa hiyo itakabidhiwa kwa Rais Magufuli na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa, Ikulu Jijini Dar es Salaam saa nne asubuhi
Mapema jana mchana wakati akipokea ripoti hizo katika viwanja wa bunge mjini Dodoma, Waziri Mkuu, Mh. Majaliwa alisema, Serikali haina mchezo katika usimamizi wa rasilimali za Taifa, na kuwataka viongozi na watendaji wote waliokabidhiwa dhamana ya kusimamia sekta ya madini wahakikishe wanatimiza vyema wajibu wao.
Amesema taarifa hiyo zimewasilishwa katika kipindi muafaka na zimeonyesha dhamira ya dhati ya Bunge, kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli na Serikali yote kwa ujumla katika kulinda rasilimali za Taifa.
Akiwasilisha ripoti yake Mwenyekiti wa Kamati ya Kuchunguza Biashara ya Tanzanite, Mh. Dotto Mashaka , alisema 80% ya Madini ya Tanzanite yanayochimbwa nchini hutoroshwa nje ya nchi kwa njia ya magendo na 20% tu ndiyo inayoingizwa katika mfumo wa kodi.
Rais Magufuli Kupokea Ripoti ya Sakata la Almasi na Tanzanite Leo
0
September 07, 2017
Tags