Rais wa Ufilipino Aruhusu Mwanaye Auwaweutwa Atakapokutwa na Mihadarati

Rais wa Ufilipino Aruhusu Mwanaye Auwaweutwa Atakapokutwa na Mihadarati
Rais Rodrigo Duterte amesema ikiwa ushahidi usiotiliwa shaka utatolewa kuthibitisha tuhuma za usafirishaji dawa za kulevya ambazo zinamkabili mtoto wake wa kiume na mwanasiasa kijana ataacha auawe na kwamba polisi watakaomuua watalindwa wasishtakiwe.

Mwezi huu, mtoto wa Rais Duterte, Paolo Duterte (42) alifikishwa mbele ya Kamati ya Seneti kwenda kukanusha madai yaliyowasilishwa na mbunge wa upinzani kwamba ni mfuasi wa genge la China linalofanya uhalifu wa kimataifa ambaye alisaidia kuingiza shehena ya dawa aina ya crystal methamphetamine kutoka China.

Rais Duterte hakuzungumzia tuhuma hizo moja kwa moja bali alirejea kauli aliyoitoa mwaka jana wakati wa kampeni kwamba hakuna mtoto wake hata mmoja anayejihusisha na mihadarati, lakini ikiwa watajihusisha watakabiliwa na adhabu kali kuliko zote.

"Nilisema hapo awali: 'Ikiwa watato wangu watajihusisha na dawa za kulevya, wauawe ili watu wasiwe na cha kusema’,” alisema Duterte Jumatano katika mkutano na wafanyakazi wa serikali ikula.

"Kwa hiyo nilimwambia Pulong (jina la utani la Paolo): 'Amri yangu ni kwamba uuawe ikiwa utakamatwa. Na nitawalinda polisi watakaokuua, endapo ni kweli,” alisema.

Duterte, 72, alishinda uchaguzi mkuu kutokana na ahadi aliyoitoa ya kuendesha kampeni isiyo ya kawaida ya kutokomeza genge la wahalifu katika jamii kwa kuua hadi wasafirishaji na watumiaji 100,000.

Tangu alipoapishwa katikati ya mwaka 2016 na kuingia ikulu, imeripotiwa polisi wameua zaidi ya watu 3,800 katika opereshani ya kupambana na wanaojihusisha na mihadarati huku maelfu wengine wakiuawa katika mazingira ya kutatanisha.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad