RC Makonda ni Mbunifu na Mchapa Kazi, Pamoja na Mapungufu ya Kitaaluma Anayodaiwa Kua Nayo

Habari za asubuhi wanabodi.

Leo nitoe ya moyoni kuhusu huyu mkuu wa mkoa wa DSM.

Awali ya yote niweke wazi kwamba mimi ni mtu huru na sifungamani na chama chochote cha siasa hapa Tanzania, ninachoandika hapa ni maoni ya mtanzania wa kawaida tu.
Sina lengo la kumpaisha mtu, sina lengo la kumkejeli RC yeyote wala sitarajii kumkosoa mtu wala chama chake. Kama mtanzania naona natafakari pia ninayo haki ya kutoa maoni.

Niweke wazi kwamba tangu nimepata akili za kutambua mambo sikuwahi kuona RC anayejituma na mbunifu kama RC huyu wa DSM, ni wazi kwamba RCs wengi hukaa ofisini, huvizia mbio za mwenge na kushiriki vikao mbalimbali ambavyo huwanufaisha kwa posho, hii inafahamika, hatukuzoea kuona RC anatumia akili zake kwa kubuni vitu vyenye manufaa kwa jamii au eneo lake la utawala.

RCs walioko madarakani awamu hii wengi wao wamekua na kazi ya kupambana na watu wanaishi kwenye mapori tengefu na hifadhi za taifa, wengine wamekua wakipambana na wanasiasa wa vyama pinzani (mnawafahamu).

Nirudi kwa RC Makonda; huyu RC ni kijana ambaye naweza kusema alistahili nafasi hiyo na pengine anastahili kua waziri wa wizara hata mambo ya ndani.
RC Makonda ameonesha ubunifu wa hali ya juu, amekua akifanya hivyo kila siku, anabuni miradi na mbinu mbalimbali za kuhakikisha mkoa wake unapata mchango wake wa moja kwa moja.
Nitaje machache tu, juzi kati ametafuta wadhamini wa kugharimia miguu bandia kwa ajili ya walemavu, amebuni mradi wa kujenga ofisi za walimu (hii ni kuboresha mazingira ya utendaji na hatimaye kuboresha taaluma ya wanafunzi mkoa wa DSM), Makonda ameenda mbali amebuni operation ya kuwapima afya wakazi wa DSM bure kabisa.

Hayo ni machache kati ya mambo mengi aliyobuni na anayobuni DC Makonda.


Inawezekana kabisa kwamba wengine mkaona RC Makonda hastahili kupongezwa, mimi nasema huyu jamaa amethubutu kuonesha umma kwamba kiongozi ni VISION sio umri, tuna mikoa isiyopungua 20 Tanzania bara lakini sijaona mkuu wa mkoa anayehangaika kuweka mambo sawa kama Makonda.

Huyu RC alituhumiwa kufoji elimu, nikitazama uwezo wake na tuhuma haviendani, kuna watu walisifiwa kua na elimu nzuri, vyeti safi lakini mbona sioni wakibuni mambo kama RC Makonda? Mbona sioni PhD zao zikitumika popote? Kweli elimu ni nyanja pana.

Naishia hapa ntarudi kujazia uzi.

Najua mtakosoa na kuponda maana sio kila mtu atapenda mawazo yaliyotofauti na mawazo yake.

Nawasilisha.

Amini usiamini, ukihitimu shule ndio utaanza masomo.

By Natoka hapa

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. By Natoka hapa.:MIMI BINAFSI NAMKUBALI HUYU JAMAA YAH,HON.RC.P.MAKONDA,,NIMZALENDO WA KWELI NA NI MCHAPAKAZI WA KWELI..HIYO HAINA UBISHI WALA MJADALA..WATU KAMA HUYU WANAHESABIKA..KM-HAYATI.J.K.NYERERE(R.I.P.),EDWARD MORINGE SOKOINE,(R.I.P.),,RAIS-J.P.J.MAGUFULI,VICE.PRES.MAMA SAMIA HASSAN,PRIME MINIST.KASSIM MAJALIWA,HON.-RC.P.MAKONDA,WAZIRI WA AFYA MH.UMMY...hawa jamaa ni zaidi ya hazina km lulu ama tanzaite..tuondoe itikadi za vyama,ukabila km CHADEMA,ni chama cha wachaga.hajabu sana nchi hii..top leaders wote wa chadema ni wachaga..ZITTO.zuberi.kabwe.alikuwa anashine pale baada ya kuona si mchaga wakamtimua kwa maslahi ya chama..waasisi wao ni wachaga,kinaendeshwa kichaga chaga maslahi binafsi kwanza watz.baadae-nani anabisha??????umeona wapi km si maslahi binafs mbele ya wazalendo nyuma au baadae-watu wamehupaa mishipa ya shingo kwa kuitisha serikali hisiishtaki ACACIA oh watatushinda kesi,waachwe waendelee kuiibia rasilimali za watz..kwa vile wao washavuta ,shikishwa km hongo shwari tu..katisha taamaa,tisha serikali tolea sana povu....finally wameangukia pua na mengine mengi tu hamuoni..tukiyaorozesha hapa mpaka asubuhi...magu oyeeee,mako oyeeee...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad