RC Paul Makonda Aendelea Kufanya Kweli Mkoa wa Dar es Salaam...Sasa Ageukia Mikopo

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amezitaka manispaa zote za jiji la Dar es salaam kuacha kutoa asilimia 10 ya mapato vichochoroni kama mikopo, badala yake watenge maeneo rasmi kwa makundi yenye kuhusika na mikopo hiyo hatua ambayo itasaidia maendeleo ya vikundi hivyo.

Bwana Makonda ametoa wito huo jijini Dar es salaam alipokuwa akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa viwanda vidogo vidogo vinavyojengwa na halmashauri ya jiji katika eneo la karakana ya mwananyamala ambapo amesema utaraibu wa utoaji wa mikopo kwa wanawake, vijana na walemavu ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ambao ulikuwepo tangu awali lakini ulishindwa kuonesha mafanikio kutokana na fedha hizo kuelekezwa mahali pasipohusika jambo ambalo limepoteza dhana ya serikali ya kuyawezesha makundi hayo.

Aidha amelitaka jiji kutenga maeneo ya ujenzi wa viwanda hivyo katika kila manispaa ili kuyaweka pamoja makundi hayo huku akiahidi kuzindua soko la wafanyabishara ndogo ndogo katika viwanja vya mnazi mmoja ambalo litakuwa likifanyika mara moja kila mwezi.

Awali akizungumzia mradi huo mkurugenzi wa jiji Sipora Liana amesema katika mwaka wa fedha 2016/2017 halmashauri ya jiji ilitenga kiasi cha shilingi milion 200 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo ambao utekelezaji wa awamu ya kwanza ulianza juni mosi 2017 ambapo hadi kufikia agosti mwaka huu ujenzi wa miundombinu imefikia asilimia 95 huku ikitenga kiasi cha shilingi milion 977 kwa ajili ya mikopo pamoja na kuendelea kujenga viwanda hivyo katika maneo mengine.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad