Risasi Alizopigwa Tundu Lissu Zamnyima Zitto Kabwe Usingizi...Afunguka Makubwa

Usiku wa kuamkia leo ulikuwa mgumu zaidi kwenye maisha yangu ya kisiasa, anaeleza Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.

“Nimetumia muda mwingi nikitafakari na kumfikiria sana mwanasiasa mwenzangu, kaka yangu, mbunge mwenzangu na rafiki yangu Tundu Antiphas Lissu,” amesema Zitto katika taarifa aliyoitoa leo Ijumaa.

Lissu alijeruhiwa kwa risasi jana Alhamisi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma na sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Aga Khan mjini Nairobi, Kenya.

Mbunge wa Singida Mashariki, Lissu alisafirishwa jana usiku baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Zitto amesema, “Siku zote, katika maisha yetu ya kisiasa, hata katika mambo tunayotofautiana na kupingana nimekuwa nikiamini kwa dhati kwamba tofauti hizo haziwezi zikatufanya tukashindwa kuvuka salama kama nchi, kama Taifa.”

Amesema kilichotokea kwa Lissu jana Alhamisi ni kitendo cha kihalifu na kisichoendana na utamaduni wa ustahimilivu na udugu ambao nchi imekuwa ikisimamia.

“Kitendo kile cha kikatili kinakwenda kinyume kabisa na misingi ya utaifa wetu ambao tumekuwa tukiujenga kwa miaka 25 sasa kwa kuwa na taifa huru kidemokrasia,” amesema.

Amesema Watanzania wanaolitakia mema Taifa wana kila sababu ya kulaani na kukataa utamaduni wa kimafia kuzoeleka nchini.

“Tusimame kulaani kwani #HuuSiUtanzania,” amehitimisha Zitto katika taarifa yake.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mmhh lazima aogope

    ReplyDelete
  2. Waswahili wanasema mganga akijifanya anajua sana na kuvuka mipaka si ajabu jamii ikamshuku kuwa ni mchawi. Tunamuombea Tundu Lisu afya njema lakini hisia zilizojengeka kwa watanzania wengi kuwa ni msaliti wa Taifa ni miongoni mwa mambo ya hatari kwa usalama wake binafsi.

    ReplyDelete
  3. NAKUMBUKA WAKATI WA MJERUMANI ANAONDOKA TANZANIA YETU. ALITUACHIA MABOMA MENGI.
    ALIVYOKUJA MN'GELEZA WAKAANZA KUTUFUNGULIA SHULE AMBAZO KITU CHA KWANZA WALIKUWA WANASISITIZA
    HELLER IS NO MORE ITS SCHILLING ( KUONESHA NEW SHERRIF IN TOWN)
    NNACH KUMBUKA VIZURI SANA NA MPAKA LEO NNAWAKANYA VIJUKUU NA VITUKUU NI HILI LA HAPA CHINI TOKA KWA MR TURNBULL (MWALIMU WANGU/WETU) USED TO WARN US.

    MIND YOUR TOUNG
    AS IT WILL LEAD TO YOUR ACTIONS
    AS SUCH IT WILL BE YOUR BEHAVIOUR
    HENCE YOUR SELF CHOSEN DESTINY.
    SO ALWAYS BE CAREFUL ON WHAT YOU UTTER AND THE AUDIENCE YOU TARGET.
    WATANZANIA TUNAHITAJI UZALENDO WA HALI YA JUU NA UPENDO.
    MUNGU LIBARIKI TAIFA LETU NA VINGOZI WAKE WENYE UCHUNGU NA NCHI YETU.
    NA UMEPE UMURI MREFU BABA JPM KUTUTUMIKIA NA KUILETA TANZANIA MPYA.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad