Roma, Stamina na Khaligraph Jones Kuachia Wimbo wa Pamoja

Roma, Stamina na Khaligraph Jones Kuachia Wimbo wa Pamoja
Wakali wa muziki wa hip hop Bongo, Roma na Stamina ‘Rostam’ wameingia studio kufanya kazi na rapper Khalighraph Jones kutoka nchini Kenya.

Rostam ambao walienda nchini humo kwa ajili ya ziara yao ya kimuziki wameweka picha pamoja na video katika mitandao wakielezea kuna ngoma inakuja kati yao na Khalighraph Jones.

Hiyo juzi katika mahojiano na kituo cha Radio Maisha Stamina alieleza rapper wa Kenya ambao anawakubali na kufuatilia kazi zao na miongoni mwao alikuwa ni Khalighraph Jones na kwa pamoja waliaidi kutoondoka nchini humo bila kufanya kolabo na msanii yeyote.

“Nawakubali wote, napenda sana kazi zao, napenda sana kazi za Octopizzo, napenda kazi za King Kaka, napenda kazi za Khalighraph lakini changuo ni kwa King Kaka,” alisema Stamina.

Kwa upande wake Roma alieleza mipango ya albamu ya Rostam kukamilika, “hadi sasa tuna nyimbo nane, tuna wimbo na Beka Flavour, Ben Pol na wasanii wengi, so before 2017 hajaisha tutatoa hii albamu,” alieleza.

Khalighraph Jones ameshafanya kazi na wasanii kadhaa kutoka Bongo akiwemo Rayvanny, Christian Bella na Rosa Ree.




Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad