Rungwe Afunguka Baada ya Kuachiwa kwa Dhamana Baada ya Kukaa Selo Kwa Siku Nane

September 6 2017 Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam liliamchia kwa dhamana, mwenyekiti wa chama cha ukombozi wa umma ‘CHAUMMA’ Hashim Rungwe baada ya kumshikilia kwa siku 8 kwa kile kilichodaiwa kuhusika katika utapeli wa Dola za Kimarekani 30,800 ambazo ni sawa na Tsh Milioni 73 kwa nyakati tofauti akiwa kama Wakili anayeendesha biashara kati ya raia wa Uturuki Ally Riza Bilgen na Kampuni ya Les Tropiques Group Mining SPRL Limited.

Inaelezwa kuwa raia huyo wa Uturuki alikuja Tanzania kwa lengo la kununua korosho tani 15 na kuandikishana mkataba wa malipo ya Dola 72,000 kama gharama za bidhaa hiyo na usafirishaji lakini tangu wamesainishana mkataba huo November 2016, hakuna kilichofanyika na malipo hayo ya awali yalifanywa kwenye akaunti ya Rungwe katika Bank ya CRDB.

Angalia VIDEO Akielezea:

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad