Serikali ya Tanzania imejipanga kuongeza vituo 150 nchini kwa ajili ya kutoa huduma ya uzazi wa dharura ili kuokoa vifo vinavyotokana na uzazi pingamizi nchini.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, katika kikao cha wabunge wa klabu ya uzazi salama kilichofanyika Mkoani Dodoma.
"Sisi awamu ya tano katika mwaka wetu huu mmoja tutaongeza vituo 150 katika kufanikisha uokoaji huo serikali pia imeandaa fedha kwa ajili ya kujenga vituo vitano vya kuhifadhia damu salama kwa ajili ya upasuaji wa akina mama wanaojifungua", amesema Waziri Ummy.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa klabu hiyo ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,Ajira, Vijana na wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama ametaka usimamizi wa fedha katika vituo vya Afya katika halmashauri zitumike kwa matumizi yaliyopangwa na wala isiwe vinginevyo.
Kwa taarifa zaidi msikilize hapa chini Waziri Ummy Mwalimu pamoja na Waziri Jestina Mhagama wakiongelea suala la kuongeza vituo vya afya ili kuweza kuokoa vifo vinavyotokana na uzazi.
play stop mute previous next
play stop mute previous next