Serikali Yapiga Marufuku Watu Kusafiri

Serikali Yapiga Marufuku Watu Kusafiri
Serikali ya Cameroon imepiga marufuku mikusanyiko ya wazi pamoja na kusafiri katika jimbo ambalo wakazi wake wengi hutumia lugha ya kingereza kuongea, kuelekea maandamano ambayo yamepangwa kufanyika kesho ya kutaka kujitenga kwa eneo hilo.

Jimbo hilo la kusini magharibi lililopo mpakani mwa Nigeria limezuiwa pia kwa watu kuingia ambao wanaonekana kuwa ni tishio kwa umoja wa taifa hilo la Cameroon.
Maandamano ya kuunga mkono ya kujitoa kwa jimbo hilo yamepangwa kufanyika kesho ikiwa ni siku ya maadhimisho ya miaka 56 ya umoja wa Cameroon, kwa kile kinachodaiwa kwamba watu wanaoongea kiingereza wengi wao wamekuwa wakibaguliwa kutopata nafasi kubwa za ajira serikalini na kwamba lugha ya kifaransa na mfumo wa kisheria imewekwa dhidi yao kuwa kandamiza.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad