Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, na kusema baada ya ajali hiyo askari hao walikosa mahali pakuishi, hivyo wanaishukuru TBA kwa msaada huo.
"Ule moto umeteketeza kila kitu kabisa, hivyo wale askari hawakuwa na sehemu ya kuishi, jana tuliwahifadhi kwenye bwalo letu la polisi, lakini leo wamepatiwa msaada na wakala wa ujenzi wa serikali (TBA ), wamepewa nyumba za kuishi kwa muda hadi pale watakapopatiwa makazi rasmi, tunashukuru kwa hilo", amesema Kamanda Mkumbo.
Tukio la kuteketea kwa nyumba hizo limetokea usiku wa Septemba 27 mwaka huu majira ya saa mbili na kuteketeza nyumba hizo, lakini jeshi la zimamoto liliwahi eneo la tukio na kutoa msaada kwa wananchi ambao walianza kuzima.