Katika kesi hiyo, shahidi wa tano, Maria Rugalabumu (63) amemueleza Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha kuwa yeye ni Sektretari wa Manji (Katibu Muktasi) na Ofisi ya Quality Group Ltd.
Akiongozwa na Wakili wa utetezi Hajra Mungula, amedai kuwa anafanya kazi katika kampuni hiyo tangu mwaka 1994 hadi sasa, wakati huo Manji akiwa anasoma.
Alipoulizwa na Wakili Mungula kwamba anamfahamu vipi Manji, amesema anamfahamu tangu anasoma na kwenye masuala ya kazi anamfahamu tangu 1997 baada ya kurithi mikoba ya baba yake.
Pia alipoulizwa kama kuna vitu vya Manji huwa anavitunza, akajibu ndio ambapo miongoni mwa vitu anavyomtunzia ni Sigara.
Aidha, amedai kuwa anashangazwa kusikia kuwa Manji anatumia dawa za kulevya hali ya kuwa amemfahamu takribani miaka 19 akisema kuwa majukumu yake ni uangalizi wa ofisi yake na ya Manji, pia kuchapa barua, kupokea wageni na kutuma barua zinazotoka ofisi yao na kusema kuwa Manji ni mchapakazi na anaweza kufanya kazi kwa muda mrefu na huwa anapenda kazi zake.
Shahidi huyo, amedai kuwa amemfahamu tangu Manji anasoma Chuo, pia alivyoanza kufanya kazi kwa Baba yake na kuieleza Mahakama kwamba yeye ndiye aliyetoa kopi ya nakala ya dawa za Manji kutoka kwa Dokta wake Marekani.
Nakala hiyo aliipata kwa njia ya e-mail, ambapo baada ya kuitoa nakala alimpatia askari ili ampe Manji ambaye alilazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, hivyo anaomba Mahakama ipokee kama sehemu ya kielelezo.
Hata hivyo, Wakili wa Serikali Mkuu, Timony Vitalis alipinga kupokelewa kwa barua hiyo kwa sababu haina uthibitisho wa kiuhalisia na daktari aliyeituma.
Baada ya kueleza hayo Hakimu Mkeha alitoa uamuzi ambapo alikubaliana na Wakili Vitalis, ambapo alisema Mahakama haiwezi kupokea kielelezo hicho.
Anaitumia dawa za kulevya anakuwa hivo? au muna yenu jamani ogopeni mungu sio munafhukumu watu bila hatia yoyote muna wazingizia na wat qneye kutumia mumewaacha munamuonea hio ni dhuluma
ReplyDelete