Silinde Afunguka Sababu Iliyopelekea Wabunge wa Upinzani Kususia Kuapishwa Wabunge 7 wa CUF

Silinde Afunguka Sababu Iliyopelekea Wabunge wa Upinzani Kususia Kuapishwa Wabunge 7 wa CUF
Mbunge wa jimbo la Momba (CHADEMA) Mheshimiwa David Silinde amefunguka na kutoa sababu kuu iliyopelekea wabunge wa upinzani leo kususia zoezi la uapishwaji wa wabunge saba wa CUF na kusema wao wamefanya maamuzi hayo kupinga bunge kutumika na serikali

Silinde amedai kuwa Bunge hilo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekuwa likikandamizi upinzani lakini pia limekuwa halifuati sheria za nchi kitu ambacho wao wanaona siyo sawa ndiyo maana wameamua kususia zoezi la uapishwaji wa baadhI ya wabunge hao wa CUF.

"Kama ambavyo leo mmetuona hatujaingia wakati wa kuapishwa kwa baadhi ya wabunge na sababu kubwa ya kutoingia ni kwamba tunapinga bunge kutumika na serikali kukandamiza upinzani pili kutofuata sheria za nchi na jambo la tatu na kubwa kuliko yote ni kwamba tunawaunga mkono wabunge wote waliondolewa na hatufurahii, kuna vitu vikubwa sisi tunekuwa tukikasirika navyo kama serikali ku- entetain maamuzi katika chama ambacho kipo kwenye mgogoro kwamba unapendelea upande mmoja unaacha upande mwingine" alisema Silende

Aidha Silinde aliendelea kudai kuwa " Hiyo ndiyo tumekuwa tukipigania siku zote hatutaki bunge kuendelea kutumika tunataka kuwa na bunge imara waone mifano kama ilivyotokea kule Kenya kama mahakama inaweza kusimama peke yake tunataka na bunge letu liendelee kusimama peke yake" alisisitiza Silinde

Wabunge hao wa upinzani walirejea ndani ya ukumbi wa bunge baada ya zoezi la kuapishwa wabunge hao wa CUF kukamilika

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad