Simba na Azam Uso kwa Uso Leo Chamanzi

Simba na Azam Uso kwa Uso Leo Chamanzi
Michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kutimua vumbi leo Jumamosi kwa kucheza mechi mbili na Jumapili mechi sita katika mzunguko wa pili baada ya kusimama kwa muda wa wiki moja.

Kwa mujibu wa ratiba mpya iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) chini ya Rais Wallace Karia, timu ya Tanzania Prison FC yenye makao yake makuu Mkoani Mbeya itakuwa katika kiwanja chake cha nyumbani Sokoine ikawakaribisha wapinzani wake Majimaji FC ya kutokea Songea majira ya saa 10:00 jioni huku Azam FC ikimkaribisha wekundu wa Msimbazi (Simba SC) katika kiwanja chake cha Azam Complex kilichopo Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar e Salaam saa 10:00 jioni.

Siku ya Jumapili timu ya Njombe Mji FC itawakaribisha Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga katika kiwanja chao cha nyumbani Sabasaba, Mtibwa Sugar FC yenyewe watakichapa na Mwadui FC katika uwanja wa Manungu uliopo Morogoro, Lipuli FC itacheza dhidi ya Stand United FC katika kiwanja cha Samora mjini Iringa. Mechi zote hizi zitachezwa majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.

Vile vile Singida United FC watashuka katika dimba la Jamhuri mkoni Dodoma kuzichapa na wakata Mbao wa Mwanza (Mbao FC), Kagera Sugar FC ikicheza katika uwanja wao wa Kaitaba uliopo mjini Kagera dhidi ya Ruvu Shooting FC huku ratiba kwa siku hiyo ikifungwa na timu ya Mbeya FC ikicheza na Ndanda FC katika dimba la Sokoine mkoani Mbeya ambapo kwa mujibu wa ratiba ya Ligi kuu timu zote hizi zitacheza saa 10:00 jioni.

Kwa upande wa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara mpaka hivi sasa timu ya Simba ina pointi tatu ikifuatiwa na Tanzania Prisons, Mwadui, Azam FC, Mtibwa Sugar, Mbeya City pamoja Mbao FC zote zikiwa zinapointi sawa tatu huku Mabingwa watetezi Yanga wakiwa na alama moja na Lipuli FC.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad