Mtandao wa kijamii wa Snapchat umefunga huduma za kituo cha Al Jazeera nchini Saudf Arabia.
Snapchat ilisema kuwa mamlaka nchini Saudi Arabia ziliiomba ifunge huduma za Al Jazeea kwa kuwa ilikiuka sheria za nchi hiyo.
Qatar inaendelea na mzozo yake na Saudi Arabia, Bahrain, Misri na UAE.
Nchi hizo nne zilikata uhusiano na Qatar mapema mwaka huu na kuilaumu nchi hiyo kwa kuunga mkono Ugaidi.
Saudi Arabia ina moja ya sheria kali zaidi kwa vyombo vya habari, kwa mujibu wa makundi ya kutetea haki za binadamu.
Lakini kawaida Saudi Arabia haiipenda Al Jazera. Wakati mmoja waliitaka serikali Qatar ikifunge kituo hicho kama moja ya masharti 13 ili kuiondolea vikwazo.
Saudi Arabia ni moja na masoko makubwa zaiid ya mitandao ya kijamii eneo la mashariki ya kati itokanayo na matumizi makubwa ya simu za smart phone.