Spika Amjibu Lema Asema Bunge Haliwezi Kusimama kwa Shambulio la Lissu

Spika Amjibu Lema Asema Bunge Haliwezi Kusimama kwa Shambulio la Lissu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amejibu tuhuma za mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, na kumtaka asipotoshe wananchi, bali apeleke malalamiko yake kwenye kamati.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akiendesha bunge, na kusema kwamba bunge lina utaratibu wake kwenye kila jambo linalohusika bungeni hapo.

"Lema asipotoshe wananchi aende hadharani kwenye kamati kuzungumzia hayo, bunge haliwezi kusimama kwa shambulio la Lissu bali kanuni zinasema mbunge akifariki bunge linasimama kwa siku moja. Na iwapo Spika akiletewa jambo la maadili linapelekwa kamati ya maadili, suala la jinai linapelekwa polisi", amesema Spika Ndugai

Pia Spika Ndugai amesema suala la Tundu Lissu kuchangiwa fedha za matibabu na wabunge wakati yeye alitibiwa nje ya nchi ni kwamba matibabu ya Tundu Lissu yameenda kinyume na utaratibu wa bunge.

"Wabunge wanaopelekwa nje (India) wanapewa rufaa kutoka hospital ya Muhimbili lakini si kama alivyopelekwa Lissu", amesema Spika Ndugai.
Pamoja na hayo Spika Ndugai amesema anamsamehe Godbless Lema na kuwataka watu kumsamehe kwani hajui alitendalo.

Hapo jana mbunge wa Arusha Godbless Lema alimlaumu Spika Ndugai kuwa anashindwa kutetea kiti chake, kwa kuzidi kuwakandamiza wabunge wa upinzani hususan suala la kupigwa risasi kwa Tundu Lissu.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Please Please Godless Wema Do not Politicise the TL na Majambazi to Become a National Agenda.
    The Country Needs you for developmental Priorities and Non other than That.
    If you find yourself Do not Fit Inn. The Door is Open Uanzishe Biashara Ya Mtori.
    Wawaha Wakusaka Milimo Mkulu alibaho aiona Milimo .
    Gwe Gwe Ubite Ukagone mdodo Ukusaka Mbeyu.
    Godless Amka tena Amka sasa hii Sio Tanzania Ile iliyokuwa Inachezea .
    Tumepata Jemedari tumpe ushirikiano na kama huwe Achia Kamba Vioja Vyenu Vinatukera na HATUVITAKI.

    ReplyDelete
  2. Please Please Godless Wema Do not Politicise the TL na Majambazi to Become a National Agenda.
    The Country Needs you for developmental Priorities and Non other than That.
    If you find yourself Do not Fit Inn. The Door is Open Uanzishe Biashara Ya Mtori.
    Wawaha Wakusaka Milimo Mkulu alibaho aiona Milimo . Zwalili Chilo Chanala Kwa Godibless.
    Gwe Gwe Ubite Ukagone mdodo Ukusaka Mbeyu.
    Godless Amka tena Amka sasa hii Sio Tanzania Ile iliyokuwa Inachezea .
    Tumepata Jemedari tumpe ushirikiano na kama huwe Achia Kamba Vioja Vyenu Vinatukera na HATUVITAKI.

    ReplyDelete
  3. Please Please Godless Wema Do not Politicise the TL na Majambazi to Become a National Agenda.
    The Country Needs you for developmental Priorities and Non other than That.
    If you find yourself Do not Fit Inn. The Door is Open Uanzishe Biashara Ya Mtori.
    Wawaha Wakusaka Milimo Mkulu alibaho aiona Milimo . Zwalili Chilo Chanala Kwa Godibless.
    Gwe Gwe Ubite Ukagone mdodo Ukusaka Mbeyu.
    Godless Amka tena Amka sasa hii Sio Tanzania Ile iliyokuwa Inachezea .
    Tumepata Jemedari tumpe ushirikiano na kama huwe Achia Kamba Vioja Vyenu Vinatukera na HATUVITAKI.
    tuliwazoea lakini hamzoleleki.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad