Mazungumzo kati ya Kamati Maalum iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na timu ya kutoka Barrick Gold Corporation yameendelea leo Jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yanafanyika kufuatia uchunguzi uliofanywa na tume mbili zilizoundwa na Mhe. Rais Magufuli kuchunguza biashara ya madini ya dhahabu na kubaini uwepo wa upotevu mkubwa fedha katika biashara ya makinikia ya dhahabu ambayo husafirishwa kwenda nje ya nchi.
Wakati mazungumzo hayo yanaendelea wananchi wanataarifiwa kuwa na subira na watajulishwa mara baada ya mazungumzo hayo kukamilika ama kwa hatua yoyote itakayofikiwa.
Kamati Maalum ya Tanzania inayofanya majadiliano na timu kutoka Barrick Gold Corporation inaongozwa na Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Palamagamba Kabudi.
Asanteni kwa Taarifa.
ReplyDeleteKazi Njema...!!!
Magu Baba, hongera Sana hoja ulikuwa nayo na Magumashi Akashi imeshzikwa Ttwiga imezaliwa na ni ya Ubia 50/50%
ReplyDeleteBARICCK NA TANZANI.
PROF.WAIMANYILE MILIMO VISWANO SANDENYI KABUDI