Taifa Hili Limepigwa Sana Kupita Maelezo Kutokana na Mikataba na Usimamizi Mbovu

Mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi ya biashara ya madini Mhe. Mussa Azzan Zungu amesema kilichopelekea taifa kulizwa kila leo kuhusiana na biashara ya madini ni kutokana na kuwepo na mikataba mibovu ambayo imetolewa nje ya nchi na kuja kusainiwa.

Mwenyekiti wa kamati ya Spika iliyochunguza uchimbaji wa Almasina Tanzanite, Mhe. Azzan Mussa Zungu.

Mhe. Zungu ameeleza hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa fupi kwa Rais Magufuli katika yale yaliyofanywa na kamati ya uchunguzi wa madini ya Tanzanite na Almasi uliofanywa na kamati maalum mbili zilizoundwa na spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai.

"Taifa hili limepigwa sana, kama lingeweza kusema lingesema nimepigwa sana na kitu pekee kinachotupiga ni mikataba mibovu, mkataba huu tumegundua kwa kauli ya IG anaamini imetoka nje na kuja kusainiwa tu hapa kwetu. Kwa hiyo maneno ya muwekezaji ndiyo yametupiga lakini laiti wataalamu na wachimbaji wa serikali wangekataa sidhani kama mgodi huu ungeharibika maana mgodi siyo mapapai kwamba yasipochimbwa yataoza, wataalamu wapo lakini wameshindwa kutumia utaalamu wao katika kusaidia taifa hili", amesema Zungu.

Aidha, Mhe. Zungu amesema watu pekee waliyoweza kuingiza nchi katika hasara kubwa ni wale ambao waliodhaminiwa na wananchi pamoja na serikali katika kulinda rasilimali hizo za nchi.
"Watu walidhaminiwa ya kulinda mali na wamekula kiapo mbele yako lakini bado wamekuwa wakipoteza mali za nchi, kwa hiyo Mhe. Rais kazi uliyokuwa nayo sisi tupo nyuma yako kukuunga mkono kwenye hilo. Mhe. Rais bodi ambayo ndiyo yenye dhamana kubwa ya kusimamia rasilimali za nchi ili wasaidie nchi iweze kupata mapato yake lakini wao wamekuwa wakiuwangusha mgodi huu tokea uwanze kwa kutosimamia vyema mali za watanzania", amesema Zungu.

Pamoja na hayo, Mhe. Zungu ameendelea kwa kusema "kamati hizi mbili za Almasi na Tanzanite zilizoundwa na Mhe. Spika ni wabunge ambapo ndani yake kuna watalamu na wenye ujuzi mbalimbali lakini hawana utaalamu mkubwa kama baadhi ya watu ambao wapo kwenye bodi waliyosomea mambo ya madini. Mhe. Rais huwezi kuamini 'chairman of audit committee' anavyoulizwa juu ya gharama za kuendesha mgodi anazipitia vipi na kuzihakiki vipi anakujibu alikuwa hana muda wa kulifanyia hilo kwa kuwa anaamini kile alichokuwa analetewa na watendaji wa chini", amesisitiza

Kwa upande mwingine, Mhe. Zungu amewataka watu watumbue kwamba vita ya biashara ya madini siyo ya Rais peke yake bali ni ya watu wote kwa kuwa mali ni za watanzania na zinapaswa zibakie Tanzania.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad