Tanzania Yashuka Viwango vya FIFA

Tanzania Yashuka Viwango vya FIFA
Viwango vya soka duniani kwa mwezi August vimetolewa leo Septemba 14 na shirikisho la soka la Kimataifa FIFA ambapo Tanzania imeshuka kwa nafasi tano licha ya kushinda mchezo wake wa kirafiki wa kalenda ya FIFA dhidi ya Botswana.

Taifa Stars sasa inashika nafasi ya 125 ikiachwa mbali na nchi za Kenya na Uganda ambazo zipo ndani ya nchi 100 bora. Uganda ambayo imecheza michezo miwlli ya kuwania kufuzu kombe la dunia 2018 dhidi ya Misiri na kushinda mchezo mmoja ikipoteza mmoja imepanda kwa nafasi mbili na sasa ianshika nafasi ya 71.

Nchi ya Kenya ambayo nayo inatoka ukanda wa Afrika Mashariki imeshuka nafasi 6 na sasa ipo nafasi ya 88 wakati Rwanda imepanda kwa nafasi moja hadi 118. Misri ndio inaongoza Afrika ikiwa katika nafasi ya 30 baada ya kushuka nafasi 5. Katika orodha hiyo Ujerumani imerejea kwenye namba 1 baada ya kuipiku Brazil ambayo imeshuka hadi nafasi ya 2.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad