Rubani wa shirika la ndege la Etihad amefariki dunia ghafla muda mfupi baada ya kurusha ndege ya mizigo ya shirika hilo.
Rubani huyo aliyekuwa anaendesha ndege ya mizigo yenye namba EY927 ya shirika la Etihad alishikwa na homa ya ghafla kitu ambacho kiliirazimu rubani wa pili kufupisha safari hiyo kutoka Abu Dhabu kwenda Amsterdam na kulazimika kutua Kuwait kwa dharula.
Shirika hilo la Etihad limethibitisha taarifa hizo kupitia kwa msemaji mkuu wake ambaye hata hivyo hakutaja jina la rubani, umri wala uraia wake.
“Baada ya kampteini wetu kudondoka ghafla ilimlazimu rubani wetu msaidizi kufanya mawasiliano ya haraka ili kuweza kutafuta msaada wa kutua nchini Kuwait, tumesikitishwa na kifo chake na kampuni yetu inaungana na familia yake kuwafariji“,imeeleza taarifa iliyotolewa jana (Jumatano) na shirika hilo kupitia kwa msemaji wa kampuni ya Etihad.
Tukio hilo limetokea ikiwa ni miezi sita tu imepita tangu rubani wa ndege wa shirika la ndege la Marekani kuumwa ghafla na kulazimika ndege hiyo kutua kwa dharula.