Dkt. Kilimbe amebainisha hayo wakati alipofungua warsha na vyombo vya habari vya mtandaoni 'online media' na kusisitizia kuwa kutokana na ukuaji wa mitandao ya kijamii ni vyema ikatumika vizuri na kuzingatia utu pamoja na staha.
"Mawasialiano ya mtandao (online) yameendelea kukua mpaka sasa kuna 'online TV' zaidi ya 50 na 'blogs' zaidi ya 150 huku TV zikiwa 32 tu hivyo ni vyema zikatumika vyema bila kufanya uchochezi wa aina yeyote", amesema Dkt. Kilimbe.
Aidha, Dkt. Kilimbe amesema kutokana na ukuaji wa mitandao ya kijamii umeweza kuonesha jinsi teknolojia ilivyopokelewa vizuri kwani taarifa zimeweza kupatikana kwa haraka endapo ukiwa na simu ya mkononi.
"Kutokana na mapokeo mazuri inabidi mitandao hii itumiwe vizuri kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa. Pia nashauri iwepo sera na kanuni za kufanikisha mitandao hii itumike vyema kimaendeleo na ndiyo maana serikali imeamua kuja na maboresho ambayo yatakuwa bora na salama, pia TCRA itakuwa bega kwa bega" amesema Dkt. Kilimbe.
Kwa upande mwingine, Dkt. Kilimbe ametoa wito kwa wale ambao hawajajiunga na chama cha Tanzania Bloggers Network (TBN) kufanya hima kujisajili kwani ni vyema kuwa na chombo kinachosimamia masuala yanayowahusu na kuwakutanisha pamoja.