Jaji Mkuu wa Tanzania, Ibrahim Juma amesema kuwa tukio la Mhe. Lissu la kupigwa risasi na watu wasio julikana ni uhalifu sio mdogo huku akisema kuwa ushahidi wa tukio hilo utakusanya hapa hapa Tanzania.
Jaji Mkuu, ameyazungumza hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuwa asikudanganye mtu kuwa mtu atatoka nje kuja kukusanya ushahidi huo.
“Tukio la Lissu ni la kihalifu nadhani tumekubaliana uhalifu mkubwa, sio mdogo ni jaribio la kuua lakini kitu cha kwanza ni kukusanya ushahidi na huo ushahidi utakusanywa hapa hapa Tanzania, asikudanganye mtu kwamba mtu atatoka nje atakusanya ndio atakuwa na uwezo wa kukusanya ushahidi , ushahidi tunakusanya hapahapa,” amesema Jaji Mkuu Juma.
Hata hivyo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wiki kadha waliomba uchunguzi wa jambo hilo ukusanywe na watu kutoka nje ya nchi na si hapa Tanzania.