Tukio la Tundu Lissu Lawafanya Wabunge Waondoe Tofauti zao...Wamchangia Milion 43 za Matibabu

Wabunge wamekubali kuchangia nusu ya posho yao kwa siku moja kuchangia matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyelazwa katika Hospitali ya Aga Khan mjini Nairobi, Kenya.

Spika wa Bunge, Job Ndugai aliwaomba kuchangia fedha hizo na wabunge wakapiga makofi kuashiria kukubali.

Hakuna kiwango kamili kilichotangazwa kama malipo ya wabunge kwa siku ambayo yameainishwa kwa uwazi lakini baadhi ya wabunge wanataja kuwa posho ya kikao ni Sh220,000 hivyo nusu yake ni Sh110,000 hivyo kuwezesha kukusanywa zaidi ya Sh43 milioni.

Lissu alishambuliwa jana Alhamisi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.

Spika Ndugai akizungumzia safari ya Lissu Nairobi amesema lilikuwa ni ombi maalumu kutoka kwa wanafamilia na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.

Spika Ndugai amewaomba wabunge na Watanzania kutulia na kuendelea kumuombea Lissu badala ya kuendelea kulaumiana kupitia mitandao ya kijamii.

Amsema tukio hilo ni la kwanza na la aina yake kutokea tangu Bunge lilipohamia Dodoma na hasa katika kipindi ambacho Bunge linaendelea na vikao.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Safi kitu gani? Hawa sapuuzi awastahili kulipwa posho 220,000 wakati wananchi wanalala njaa

    ReplyDelete
  2. Wameonyesha utu kuweka tofauti pembeni...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Utu kwanza watakiwa wao yeshe kila siku kwa wananchi waliowachagua na kulipa kodi sio baadhi yenu mnatuma watu wamshambulue mwenzenu halafa wote mnajifanya amjui na kuanza kuchangia huo ni unafiki sio utu

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad