Tunda la Tikiti Maji na Kuongeza Nguvu za Kiume

Tunda hili lina faida nyingi pamoja na kuwa ni chanzo kikuu cha Protini, Mafuta, Nyuzinyuzi, Wanga, Calcium, Phosphorus, Chuma,Vitamin A, B6, C, Potasium, Magnesium, Carotene, anthocyanins na Virutubisho vingine vingi.

Tunda hili linasaidia kuwa na uwezo mkubwa wa kuimalika kwa misuli na mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri na kukuondoa katika hatari ya kupatwa na shinikizo la juu la damu.

Tikiti maji na nguvu za kiume

Tafiti za karibuni zinasema karibuni zinaonyesha kila wanaume watatu mmoja na ana tatizo la kupungua kwa nguvu za kiume na dalili zinaonyesha idadi itaongezeka mara mbili miaka ya karibuni.

Kwa bahati nzuri madaktari na watafiti mbalimbali wameendelea kufanya utafiti juu ya suluhisho la tatizo hili kwa njia salama zisizo na madhara mengine baadaye.

Tikiti maji linasemwa kuwa ni mkuyati wa asili pia kama lilivyo parachichi. Kwenye tikiti maji kuna vitu hivi vitatu mhimu sana kwa afya ya mapenzi navyo ni ‘lycopene’, ‘beta-carotene’ na ‘citrulline’ ambavyo husaidiwa kuweka mishipa ya damu katika hali ya utulivu.

Tikiti maji ni viagra ya asili inayoweza kutumika kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa watu wa jinsia zote mbili bila kukuacha na madhara yoyote mabaya.

Kwenye tikiti maji hasa mbegu zake kuna kitu kingine kinaitwa ‘L-arginine’ ndicho ambacho huhusika na kuongeza nguvu za kiume. Mbegu za tikiti maji zimeonyesha matokeo mazuri katika kuimarisha nguvu za kiume hata kwa wazee kabisa.

Unachohitaji ni kula tikiti maji kila siku sambamba na mbegu zake na hutakawia kuona tofauti.

Faida nyingine 27 za tikiti maji kiafya

Asilimia 92 yake ni maji
Vitamini A ndani yake huboresha afya ya macho
Vitamini C ndani yake huimarisha kinga ya mwili
Huponya majeraha
Hukinga uharibifu wa seli
Huboresha afya ya meno na fizi
Vitamini B6 husaidia ubongo kufanya kazi vema
Hubadilisha protini kuwa nishati
Chanzo cha madini ya potasiamu
Husaidia kushusha na kuponya shinikizo la juu la damu
Hurahisisha mtiririko wa damu mwilini
Huondoa sumu mwilini
Huongeza nguvu za kiume hasa ukila pamoja na mbegu zake
Tunda zuri kwa mwenye Kisukari aina ya pili
Husafisha figo
Huzuia na kutibu kansa mbalimbali
Tunda zuri kwa mwenye ugonjwa wa moyo
Huzuia na kutibu pumu
Hutibu tatizo la kufunga choo
Hufanya ngozi ing’ae
Huhamasisha kuota nywele
Husaidia kupunguza uzito
Huimarisha mifupa
Husaidia kuponya vidonda na majeraha
Huzuia madhara yasitokee katika seli
Huzuia ugonjwa wa baridi yabisi ya moyo (heart stroke)
Hutibu kiseyeye (scurvy)

By Fadhili Paul
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad