Tundu Lissu Ametangazwa Shujaa Huko Lagos Nchini Nigeria Magharibi mwa Bara la Afrika
4
September 16, 2017
Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tundu Lissu, ametangazwa katika kongamano la kimataifa lililofanyika jijini Lagos, nchini Nigeria, kuwa ndiye mwanasiasa kiongozi katika kutetea matumizi mazuri ya raslimali za taifa lake,anaandika Jabir Idrissa.
Wanakongamano waliokusanyika kujadili amani duniani, wamesema: “Lissu ni kielelezo kizuri cha kiongozi mwenye maadili na shujaa wa haki za binadaamu… mpenda haki na mwanasiasa mkweli anayestahiki kuombewa na wapenda amani hata kufikia kuwa rais katika nchi yake.”
Kwa ujasiri wake katika kukataa dhulma na kuitumia vema fani ya sheria katika kusimamia raslimali za taifa lake, wanakongamano wamesema, “mamilioni ya vijana duniani kote wameanza kuomba kusoma fani ya sheria vyuoni baada ya mitandao ya kijamii zaidi ya 11,000 kuripoti habari zake kwa muda wa siku 11 mfululizo kuliko habari za rais yoyote duniani.”
Taarifa zilizofikia MwanahalisiOnline kutoka Nigeria, zimesema hatua hiyo imefikiwa kwenye kongamano lililomalizika jana likishirikisha vijana wasomi wa Kikristo kutoka vyuo vikuu 283 vya Afrika, Marekani, Asia na Ulaya waliokubaliana kuwa Lissu ni kielelezo kizuri cha kiongozi mwenye maadili na shujaa wa haki za binaadamu.
Profesa Bigs Ezziel kutoka Marekani ambaye katika kongamano hilo la siku tano alifundisha mada ya HAKI, ameonya kuwa nchi nyingi za Afrika bado hazijui thamani ya haki ambayo ndiyo tunu nguzo kuu ya amani na demokrasia.
Akimzungumzia Lissu, Prof. Ezziel alisema wamefuatilia kwa karibu habari za mwanasiasa huyo na kuridhika kuwa ni mtu wa pekee kwa kusema ukweli. “Kwenye Balozi zetu wamekuwa wakituletea mambo yote pale Tanzania bila ya shaka anatakiwa apewe tuzo maalum ili kuwachochea vijana wa kizazi hiki kukataa dhulma.”
Prof. Ezziel ameshauri wasomi wa sheria katika nchi za Afrika kumualika Lissu kwenye vyuo vyao ili atoe elimu itakayowezesha wasomi kuielewa fani ya sheria kwa mapana yake kuliko ilivyo sasa kukikosekana tija hasa ya wanasheria katika nchi zao.
“Ni muhimu tutambue kuwa HAKI ni nguzo muhimu kwa amani, upendo na maendeleo. Mwenyezi Mungu anajitambulisha waziwazi kuwa yu Mungu wa haki… inasikitisha wanasiasa wengi barani Afrika wapo kama mafisi kwa kutamani madaraka badala ya kutamani kumtambua Mungu kwa kufanya yale yanayojenga jamii zao.
“Badala yake wanatumia siasa za kugawa wananchi huku wakitumia nguvu za dola kuharibu amani na utulivu katika nchi zao. Tanzania inakwenda vibaya kutokana na wanasiasa kutoenenda katika kuonesha ni kielelezo cha maadili kama alivyokuwa Mwalimu Nyerere ambaye hakutaka kujilimbikizia mali wala kupenda kutumia nguvu za dola kuonea wananchi,” alisema.
Amehimiza viongozi wa kiroho barani Afrika kumuomba Mwenyezi Mungu kulisaidia taifa la Tanzania ili kulinusuru na balaa linaloweza kutokea kutokana na maongozi yanayokiuka haki za binaadamu huku wakimuombea Lissu, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baraka ili kutimiza ndoto yake ya kuona maliasili na raslimali za Tanzania zinanufaisha Watanzania.
Amesema Afrika inahitaji mabadiliko makubwa kisiasa, tofauti na siasa zinazoshuhudiwa zama hizi kwa marais kunogewa na madaraka hata kujifanya Miungu watu. Waruhusu mawazo ya wengi kutawala badala ya kauli ya mtu mmoja kuongoza taifa la mamilioni ya watu. Huko ni kumkataa Mwenyezi Mungu ambaye humsikiliza na kumlisha kila mtu na kila ndege wa angani.
Prof. Ezziel, mwanasheria na mshauri wa sheria kwenye vyuo vikuu 17 vya Palestina, Djibouti, Ghana, Marekani na Jerusalem, amepongeza wanasheria wa Tanzania kwa kumchagua Lissu kuwa rais wa jumuiya ya wanasheria ya Tanganyika. Uamuzi wao wakati wa mkutano mkuu wa Tanganyika Law Society (TLS), amesema umewapata kuheshimika duniani.
Kadhalika, Lissu ametajwa na Dk. Marucus Bahod na Dk. Chris Zulu kuwa “mwanasiasa wa mfano katika karne hii” ambaye ameifundisha dunia umuhimu wa kusimamia haki na sheria na kuifanya taaluma ya sheria kung’aa kwa muda mfupi kiasi cha kusababisha macho yote ya wanazuoni duniani kuiangalia Tanzania kwa kumfuatilia Lissu.
“Ni mwanasheria anayejiamini kutetea matumizi mazuri ya raslimali na maliasili za taifa lake bila ya kujali nguvu kubwa inayotumika na serikali kumkatisha tamaa… mwanasiasa anayeweza kuiongoza Tanzania kwa uwezo wake wa kimaadili na kuitafsiri sheria kwa faida ya Watanzania wote.
“Ni mfano mzuri kwa wanasheria wengine Afrika ambao wanakuwa wazito kusimamia matumizi ya manufaa ya maliasili katika nchi zao na hivyo kuzinyima fursa za maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Kutokuwa mbele katika kutetea maliasili za mataifa ya Afrika kunachangia kuua demokrasia, utawala wa haki na sheria,” alisema.
Madaktari hao walisema ni vema wanaotafuta uongozi wa kisiasa barani Afrika wawe watu wema na kamwe wasiruhusu watu wenye visasi kupewa dhamana ya uongozi kwani wakishapata madaraka, huzalisha chuki na fitna katika jamii badala ya maendeleo.
Askofu William Muller kutoka Ujerumani, aliongoza dua ya kuiombea Kenya kuendelea na amani wakati na baada ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi huu. Nazo nchi za DR Congo, Tanzania, Afrika Kusini, Msumbiji, Ghana, Nigeria, Uganda, Burundi na Gabon zimeombewa ili zirudi kwenye maendeleo makubwa ya kiuchumi.
Tags
Watu wengi hukuwapa Hata nguvu wengi watachukua. Huu ndio uzalendo wa kweli. Mnapotaka kuufunika ndipo unainuliwa na nguvu za Juu. Usomi, Welevu, ushujaa, hekima, Uzalendo, Imani, Akili, Elimu, Kujitoa, Kujichagulia hivi vyote vipo. Ni Wachache sana wenye upeo wa hali ya juu. Ni kipaji toka kwa Mungu. Kuna Wanasheria wengi walimkacha Ndugu Tundu Lissu. Dunia inamwinua. Wote waoga, sasa Mtafanyaje, Wengi mmejitetea kivyenu. Busara. Si kila Msomi is well polished, very few. Wengine wana vyeo sababu tu ya Upendeleo. Havidumu, na hao ndio maadui wa kweli wa maendeleo Barani Africa hasa Tanzania kwa sasa. MMeliamsha dudu , angalieni majanga yanayoendelea kila siku. Kama Zimbabwe, au Iraqi. Leo Kabwe kachomewa moto nyumba. Hawa ni vijana shupavu wa nchi hii. Makonda anaulinzi masaa 24, hata nusu ya ubongo , elimu hakuna. Ndo mtawala wa jiji la Dar es salaam, kusaidiana na Makopo ya china. Vibaiskeli, vibodaboda ambavyo havijengi uchumi wa Dar esalaa. Nguo cheap, madeni China, vinaharibu viwanda vyetu. Wajengaji Wachina, wanachukua ajira za vijana Watanzania. Mchina anaendesha bidhaa barabarani, unataifisha bidhaa aliyoitengeneza Mtanzania. Je hii ni sawa Dereva? TAATA. Hiyo si sawa Dereva, acha vituko. Somea mambo ya uchumi. Ni bidhaa za Tanzania tu, zitengenezwazo nchini ndizo zinainua Uchumi wetu. Si madeni na makopo ya Wachina, wezi, hawatii, wanatuibia madini kila wapitako. Mnamchekea na kula naye. Mtanzania Mnyonge kodi kubwa, Huu si ujinga na mnaua viwanda nchini na kujenga viwanda vya Wachina na Wageni. Si vyenu. Je Uongozi wa sasa unajua haya?
ReplyDeleteKwa lipi lakini?
ReplyDeleteMaana masifa yamekuwa mengi bila ya kutaja ni kwa lipi hasa jamaa huyu aitwe shujaa na awe eti mfano wa kuigwa na sababu ya vijana wengi kutaka kusoma sheria.
Japo basi wangeorodhesha mifano ya aliyoyafanya katika Tanzania au hata nje ili kujengea hoja matamko yao. Wameshindwa kufanya hivyo na sishawishiki na utenzi wao uliojaa usanii wa kumsifu mtu ambaye namkumbuka katika matukio ya usaliti wa nchi yake kuhusiana na tashwishi zake katika suala la ndege zetu. Pia namkumbuka alipolisimamia kidedea suala la kumngo'a kimizengwe Zitto Kabwe katika CHADEMA, kitendo kilichokemewa na kila mpenda demokrasi ndani ya vyama vya siasa.
Ni nani amemsahau huyu mtu alipokiongoza chama chake kuonesha namna walivyo vigeugeu Lowassa alipojitoa CCM. Hawa jamaa walisafiri nchi nzima kumponda Lowasaa wa CCM kuwa mtu asiyefaa uongozi, na baada tu ya kuondoka kule huyu jamaa akaongoza watu wake kumkumbatia na kumsifu, kisha kumruhusu awe mgombea wao wa urais kinyume na katiba ya chama chao.
Ni huyu huyu aliyekiongoza chama chake kuwatukana CUF matusi ya nguoni walipokuwa wanashirikiana na serikali ya Zanzibar, kisha akageuka kuwa rafiki yao katika uchaguzi uliopita.
Jamaa huyu ni hodari wa kucheza na upepo, mkosoaji mkubwa ilhali yeye mwenyewe akishindwa kusimamia haki na demokrasia katika chama chake ambacho kinashutumiwa kwa upendeleo hata katika kuteua wabunge wa kuteuliwa ambao karibu wote wana ukaribu na viongozi wa juu.
Ni mbunge ambaye humsikii anachokifanya jimboni kwake ila kutwa kucha huwa fedhuli kutukana Serikali mjini akatafuta mabifu ya kumtengenezea jina magazetini. Ustaarabu na heshma kwa viongozi wa nchi si vitu vyenye thamani kwake, na kwangu mimi si mtu wa kuwashaeishi wanangu wamwige. Vipi msomi wa sheria asiweze kuthamini viongozi na anuke mdomo!
Habari hizi hazina kina na kwa watu kama mimi sioni uhalisia wake. Jamaa huyu tunamjua vizuri huku Tanzania. Badala ya kukaa huko nje wakafanya usanii waje watuulize tuwape taarifa za kuaminika zenye ushahidi. Historia imethibitisha kwa muda mrefu dunia haina taarifa za kutosha za wanasiasa wa Afrika.
Je hawa jamaa wametumia vigezo gani?
Au kuna ushawishi fulani nyuma ya pazia?
Watueleze.
Otherwise huu ni usanii wa kiwango cha juu na ni mzaha kwa watanzania.
Si rahisi kumfundisha, kumwamsha asiye na uwezo wa kufikiri, kuona. hata kufuatilia mambo. Kama mtu huoni hutaonyeshwa tena. Ila tu, ukae hapo ulipo. Mstaarabu nani. Nchi yenye matatizo ambayo yameletwa na dola, Kama Mtanzania haoni hataona tena. Ni dola iliyosaini mikataba, Ni dola iliyowaachia viongozi wa dola mafisadi wa ESCROW, IPTL, Inawafunga watu kutokuyaweka wazi yaliyoharibika nchini kupitia dola. Iliwatetea IPTL kwa muda mwingi ikasema hii si mali ya Umma. Tulijitengenezea Katiba ili viongozi wasipate kinga kukomesha ufisadi na mikataba mibovu haikusainiwa na Maraisi. Na haya yote ni Ndugu Lisu, Zitto Kabwe, Kafulila, Bashe, Mnyika, Mdee, Ester, Msigwa, Mboye na wengine wengi, Ndio wanaomsukuma Raisi achukue hatua. Lakini wengi hawawaadhibu. Sheria inavunjwa kila siku. Ndio wanaotufungua macho Watanzania wengi kuhusu Makinikia, Dhahabu, Almasi, Ndege zetu. Wanatufumbua macho kutuonyesha Tanzania si maskini. Bali Viongozi wetu ndo shida. Polepole watu tunaamka. Wewe usiyeona hutaona sababu hutaki kuona, au huna macho. Dunia kwa mara ya kwanza inaona na inashangaza Mtanzania kama wewe huoni. Alilolifanya Tundu lisu, ni kuwafundisha Waafrika kujua sheria zao ili Wajitetee wenyewe. Kwa mara ya kwanza wanaona Faida za elimu bora hasa Sheria ili waweze kuzifahamu haki zao na kuzipigania pale viongozi wetu wanapotupotosha. Tulilala mno, na Wengi bado wamelala. Ni elimu tu itambadili mwafrika aweze kujiamini hasa nchini kwake na kutaka haki ya kweli kwa wote, kutaka uwazi, kpigania raslimali zao na kuwa huru kifikra. Kama huoni umuhimu watu duniani wameuona kwa kufuatilia hili kupitia siasa zetu. Hakwenda nje, bali habari na ukweli wa mambo umejionyesha wenyewe na Kumpaza Lissu. Hii huwezi kupinga umeshachelewa. Nakushauri pata hasira zaidi zama kwenye vitabu ujikomboe kiakili.Hapo utafunguka macho.Hasira itakusukuma kupata ukweli vitabuni kwa kujiendeleza kimasomo.
ReplyDeleteNchi yenyewe huko alipotangazwa yaani Nigeria kumejaa kila aina ya uozo wa rushwa na utapeli hata habari za Lisu inawezekana asilimia 99% ni fake news. Kwa lipi alilolifanya Lisu la kupigania rasilimmali? Amewapigania Acacia wazidi kutorosha madini yetu kiutapeli vya kutosha labda hilo tangazo litakuwa limekuwa limelipiwa na Acacia kuwa Lisu ni shujaa.wanaouwezo huo��
ReplyDelete