Udart Yawaangukia Wateja Wake Yakiri Kutotoa Taarifa Kuhusu Tatizo Lililotokea


Udart Yawaangukia Wateja Wake Yakiri Kutotoa Taarifa Kuhusu Tatizo Lililotokea
Kampuni ya Usafiri wa Mabasi yaendayo Haraka (Udart) imekiri kufanya makosa kwa kutofikisha taarifa vituoni kwa wateja wanaotumia usafiri huo kuhusu matatizo yanayotokea kwenye mabasi hayo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Udart, Deus Bugaywa alisema hayo jana baada ya mabasi hayo kugongana eneo la Shekilango na kusababisha barabara kutopitika.

Alisema kufuatia ajali ilitakiwa abiria wapatiwe taarifa wakiwa kwenye vituo vyao, lakini haikuwa hivyo na badala yake wakawa wanashindwa kujua nini kinaendelea.

Deus alisema kilichojitokeza jana ni tatizo la kibinadamu, hivyo amewataka watu wawe waelewa.

“Kwenye kila kituo tuna watu wetu ambao tunawasiliana nao ili kuwajulisha abiria wetu pale tatizo linapotokea, lakini leo (jana) hatukufanya hivyo” alisema Bugaywa.

Pia, alisema tatizo lililopo ni mapokeo ya abiria wanaotumia usafiri huo pale wanapopewa taarifa ambapo wengi huonyesha kutofurahishwa na taarifa hizo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad