Uhuru na Makamu wake William Ruto walisema wanajivunia idadi kubwa ya wabunge walionao. Wawili hao ndio watapambana na wagombea wa muungano wa Nasa Raila (ODM) na Kalonzo Musyoka (Wiper) katika uchaguzi wa marudio uliopangwa Oktoba 17.
"Hakuna haja ya kuogopa hata akichaguliwa. Tuna idadi kubwa ya wabunge na tutamtoa Ikulu katika muda wa miezi mitatu,” alisema Uhuru.
Akizungumza Ikulu leo Jumatatu, Rais amesisitiza kwamba wana idadi kubwa ya wabunge na maseneta hivyo wanaweza kutumia wingi wao huo wakati wowote wakiona inafaa.
"Hakuna kitu cha kuhofia. Leo hii hata Raila akichaguliwa atatawala Kenya kwa njia gani. Jubilee inaweza kukamilisha biashara hata asipokuwepo seneta wa Nasa...hatuwahitaji."
Muungano wa chama tawala pamoja na vyama rafiki una jumla ya wabunge 193 katika Bunge la watu 349 na wawakilishi wanawake.
Kubadili Katiba
Kutokana na wingi huo, Uhuru amesema wanaweza hata kubadili Katiba bila mchango wa upinzani.
"Katika Bunge la Taifa, tuna upungufu wa wabunge 13 tu, hii ina maana tunaweza hata kubadili katiba bila wao. Atafanya nini huyu? Atafanya nini?" aliuliza.
Uzinduzi wa Bunge
Kuhusu kikao cha kwanza cha Bunge kesho Uhuru amesema kitafanyika hata kama wawakilishi wa Nasa hawatahudhuria.
Wabunge wa Nasa wamesema “watagoma” kuhudhuria uzinduzi wa Bunge litakalohutubiwa na Rais Uhuru.
Kiongozi wa walio wachache bungeni Opiyo Wandayi amesema hawawezi kumsikiliza Rais asiye na mamlaka.
TAZAMA VIDEO: