Utafiti uliochapishwa katika Jaida la British Journal of Psychology, ulibaini kuwa wanaume huwachukulia wanawake ambao ni warembo kama vyombo vya starehe tu.
Utafiti umeonyesha kuwa wanaume wengi wanapendelea kuwa katika mahusiano ya muda mrefu na wanawake wasiokuwa na mvuto sana ikilinganishwa na wanawake wenye mvuto (warembo).
Baadhi ya sababu kwa nini wanaume wanapendelea kuwa katika mahusiano na wanawake wenye mvuto na warembo badala ya kuwaoa ni pamoja na;
Utafiti uliofanyika hapo awali ulibaini kuwa wanawake wenye mvuto ni rahisi zaidi kutokuwa waaminifu ndani ya mahusiano hasa pale wapenzi wao wanapokuwa hawana mvuto. Wanaume wengi huwa na wasiwasi pale wanapokuwa mbali na wapenzi wao, huwa wanakuwa na maswali mengi
Wanawake wenye mvuto hutafuta umaarufu. Wanaume hupenda wanawake wasiokuwa na mambo mengi, lakini kwa upande wa wanawake warembo inaonekana kuwa wao hujali zaidi muonekano wao na mvuto wao wa nje kuliko walivyo ndani (tabia na mwenendo) hivyo kukosa sifa za kuwa wake bora. Ni vigumu sana kuendana na baadhi ya matakwa ya wanawake warembo.
Sababu nyingine ni kuwa, wanawake wenye mvuto na warembo hutajwa kuwa ghali (inahitaji gharama kubwa kummudu mwanamke wa aina hii).
Hili linaangalia zaidi aina yao ya maisha. Wanawake hawa hupendelea kuvaa nguo za gharama, kuishi maisha ya starehe na kufanya vitu ambavyo vinahitaji gharama kubwa, hivyo wao hupendelea kuwa na wanaume ambao wana kipato cha kutosha kuwahudumia mahitaji yao yote.