Upelelezi wa Kesi ya Vigogo wa TRA Waliokwepa Kodi na Kusababisha Hasara ya Bilioni 29 Bado Haujakamilika

Upelelezi wa Kesi ya Vigogo wa TRA Waliokwepa Kodi na Kusababisha Hasara ya Bilioni 29 Bado Haujakamilika
Upelelezi wa kesi ya uhujumu uchumi kwa kuisababishia hasara ya Tsh Bilioni 29 Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ inayowakabili watu watatu akiwemo Mhasibu wa Mamlaka hiyo, Reuben Mwakasa, bado haujakamilika.

Mbali na Mwakasa, mkazi wa Msagara, Moshi, Kilimanjaro, washitakiwa wengine ni Meneja wa Tema Enterprises, Ephraim Magete, mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam na mfanyabiashara Elizabeth Massawe, mkazi wa Makongo Juu.

Wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika ambapo, baada ya kueleza hayo Hakimu Mwijage ameahirisha kesi hiyo hadi October 11, 2017.

Washtakiwa hao wanadaiwa walitenda kosa hilo, kati ya November 22, 2013 na August 21, 2017, katika maeneo mbalimbali ya Wilaya za Temeke na Ilala.

Inadaiwa washitakiwa hao kwa pamoja vitendo vyao waliisababishia TRA hasara ya kiasi hicho kwa kukwepa kulipa kodi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad