Video: Vodacom Wazindua Pindua Pindua kwa Wateja Wake

Mtandao wa Simu ya Mkononi vodacom wamezindua huduma ya kifurushi kipya cha pinduapindua kwa facebook, dakika, sms bure

Pinduapindua ni kifurushi huru na cha kipekee zaidi kuliko vifurushi vingine vinavyowapangia wateja wa kampuni zingine za mawasiliano nchini,Bando hili litawapatia vijana na wateja uhuru wao wa kuchagua kiasi cha kupangia kwenye data, kupiga simu (voice) au ujumbe mfupi (SMS) kulingana na mahitaji ya wakati huo. “Pinduapindua” pia itamwezesha mteja kutumia Facebook (ikiwa pamoja na picha), Whatsapp (maandishi na picha) na SMS hadi 200 bure.


Jinsi yakupata vifurushi vya bando hili ni rahisi mteja atahitaji kupiga namba *149*01# kisha kuchagua kifurushi cha siku, cha wiki au cha mwezi. Vifurushi hivi vinaweza kulipiwa kupitia muda wa maongezi au Mpesa na mara baada ya kununua, mteja atapatiwa kifurushi chake, Facebook BURE, Whatsapp BURE na SMS, vyote ambavyo vitatumika kwa muda wote wa kifurushi alichochagua
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad