Vijana ACT Wazalendo Wafunguka.."Bunge Limepoteza Imani yake Kwa Umma kwa Kiwango Kikubwa"

Katika taarifa ya Ngome ya Vijana iliyotolewa leo September 13, 2017 kupitia kwa Katibu wa Itikadi, Mawasilano na Uenezi, Karama Kaila imeridhia Zitto Kabwe kuitikia wito na kueleza hoja tano kuhusu Bunge na mwenendo wake.

1. Bunge limepoteza imani yake kwa umma kwa kiwango kikubwa Sana.

Jambo hili lisipochukuliwa hatua za haraka na makusudi na Bunge itafika wakati kujitambulisha Kama Mbunge itakuwa ni aibu mbele ya Jamii.

2. Bunge limepoteza nguvu mbele ya serikali ndiyo maana leo taarifa ya Kamati teule ya bunge kuhusu madini imeshindwa kujadiliwa ndani ya bunge na kuwa Na maazimio badala yake imepelekwa moja kwa moja serikalini.

Kwa Jambo hili Bunge linapaswa kurudi kusimamia kanuni zake ilizojiwekea ili mambo Kama haya yasifanyike tena.

3. Bunge limeshindwa kuwapa wabunge ulinzi wa kutosha hasa kipindi ambacho Bunge linaendelea na hata linapoahirishwa pamoja na wabunge kutoa taarifa ya kuwa usalama wao upo mashakani.

Ngome ya Vijana tunaitaka Kamati ya bunge ya ulinzi Na usalama ivunjwe Na kuundwa upya.

4. Muendelezo wa wabunge kuitwa Kwenye Kamati ya maadili kwa sababu zisizo na kichwa wala miguu hakiashirii mwisho mwema na kina lengo la kuwafanya wabunge washindwe kutimiza wajibu wao wa kuisimamia serikali

Ngome ya Vijana tumeridhia Kiongozi wetu wa Chama Ndugu Zitto Kabwe kuitikia wito wa Kamati ya maadili Ila Kamati itambue kuwa maamuzi yoyote itakayochukua dhidi yake yasiyostahili Vijana wa ACT-wazalendo nchi nzima tutayapinga kwa vitendo.

5. Mwisho Kitendo cha Bunge kuridhia kuzimwa kwa Bunge kurushwa moja kwa moja Ngome ya Vijana tunathubutu kusema hapa ndipo Bunge letu lilipoamua kujichimbia Kaburi.

Karama Kaila
Katibu Itikadi, Mawasilano Na Uenezi,
Ngome ya Vijana ya ACT-Wazalendo Taifa,
13/9/2017
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad