Wafanyabiashara wa Mbolea Wabanwa

Wafanyabiashara wa Mbolea Wabanwa
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba amewataka wafanyabiashara wa mbolea kuwaweka wakulima wadogo kuwa kipaumbele badala ya kuwaza faida pekee.

Akizungumza katika mkutano wa wadau wa sekta ya mbolea leo Alhamisi, Dk Tizeba amesema asilimia 65 ya Watanzania wamejiajiri katika kilimo na hawawezi kupata faida bila kujua matumizi sahihi ya mbolea.

"Kama mkulima amewekeza Sh200,000 kwenye shamba lake halafu akavuka akapata Sh190,000 hiyo ni hasara kubwa,  lakini kama kampuni imewekeza Sh200,000 kwa lengo la kupata faida ya Sh20,000 lakini ikapata Sh18,000 si shida kwa Serikali, " amesema Dk Tizeba.

Akizungumzia bei elekezi, amesema imeshapigiwa hesabu za usafirishaji na faida, hivyo wafanyabiashara hawapaswi kuongeza faida zaidi.

"Tumeshachukua uamuzi kwenye biashara ya mbolea aina mbili, yaani DAP na Urea, bei isiwaumize wakulima. Tumeondoa tozo mbalimbali ili kila upande ufaidike ikiwezekana mkulima afaidike zaidi," amesema.

Amesema, "Nimesimama kwenye mkutano jimboni kwangu mwezi uliopita nikauliza wangapi wanatumia mbolea, hakuna aliyenyoosha mkono, nilipouliza wangapi hawatumii, wote wakanyoosha, hii haikubaliki."

Hata hivyo, baadhi ya wafanyabiashara wamesema bei elekezi ya mbolea haikuzingatia gharama halisi na haina faida.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad