Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu pamoja na wanachama wa Chama cha wamiliki wa malori Dar es salaam. |
Mwenyekiti wa cha hicho, Emmanuel Godson Moshi katikati akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda
Hatua hiyo imekuja baada ya RC Makonda kuwaomba wadau na wananchi kuchangia fedha na vifaa ikiwemo mabati, nondo, saruji, kokoto, mchanga, mbao na vguvu kazi ya watu katika ujenzi wa ofisi 402 za walimu Dar es salaam ili kuwafanya walimu wafanye kazi katika mazingira mazuri.
Akiongea na waandishi wa habari katika kikao chao walichomualika mkuu wa mkoa huyo, Mwenyekiti wa cha hicho, Emmanuel Godson Moshi akiwa pamoja na wanachama wake zaidi ya ishirini, alisema wao kama wamiliki wa malori wameamua kutoa huduma ya kubeba mchanga bure katika mradi huo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika maendeleo ya jamii.
“Mh Mkuu wa Mkoa sisi tumekuita hapa kwanza kukupongeza kwa kazi nzuri ambazo unazifanya katika juhudi za kuwaletea maendeleo wananchi wa Dar es salaam. Sisi kama chama cha wamiliki wa malori Dar es salaam tumesikia kwamba unahitaji msadaa wa vitu mbalimbali katika ujenzi wa nyumba za walimu wetu 402 Dar es salaam, kama chama chetu tumependezwa na hicho unachokifanya na tumeamua kutoa huduma ya kubeba mchaka bure katika mradi huo mpaka unakamilika, suala la mchanga tuachie sisi, sisi tutatoa malori yetu kwaajili ya kufanikisha hili suala la mchanga kabisa,” alisema Emmanuel Moshi.
Kwa upande wa RC Makonda baada ya kupokea msaada huo aliwashukuru wamiliki wa malori na kuwataka wadau wengine waige mfano kwa kuwa jambo linalofanyika ni kwaajili ya kuiboresha sekta ya elimu huku akisema hatua hiyo itakwenda kuchochea maendeleo ya elimu ndani ya mkoa wa Dar es salaam.
“Nawashukuru sana kwa sababu mmenifanya niendelee kutembea kifua mbele na kupata usingizi, hiki kitu ambacho mmekifanya nikikubwa sana kwa mkoa wa Dar es salaam, kina manufaa kwa elimu yetu kwa ujumla, kwahiyo mimi niwashukuru kwa hatua hiyo pia wadau wengine watuunge mkono kwa sababu kama tumemaliza suala la mchanga bado kuna maeneo mengine kwenye mradi huu ambayo yanahitaji pesa,”
Amesema kuwa wananchi wanaweza kuchangia fedha kupitia Account ya
CRDB namba 0150296180200 au kuwasilisha michango yao Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Ujenzi rasmi wa ofisi 402 za walimu utaanza rasmi Septemba 4 mwaka huu.
Source:Bongo5