Wananchi wa mtaa wa Fonga kata ya Pasua, mkoani Kilimanjaro wamemwomba Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendelo ya Makazi, William Lukuvi kuingilia kati bomoabomoa inayoendelea mkoani humo.
Wananchi hao walisema kuwa maeneo yaliyowekwa alama ya X yana hati miliki ambayo walipewa na Wizara ya Ardhi.
Hata hivyo mmoja wa waathirika hao, Charles Msuya amesema wao sio wavamizi na wamepewa kihalali maeneo hayo na Manispaa ya Moshi
Amesema wamekua wakilipia majengo hayo kila mwaka tangia
wamilikishwe maeneo hayo rasmi na Manispaa.
“Nikirejea nyuma, Oktoba, 2007 kipindi cha Waziri wa Ardhi wakati huo Rais John Magufuli alikuja katika maeneo yetu na kuhutubia wananchi na moja wapo ya vitu alivyoagiza ni mkurugenzi chini ya mkuu wa mkoa aliyekuepo kipindi hicho kuhakikisha wananchi wa eneo hilo wanapewa hati miliki na ndiyo watu walianza kujenga na hadi sasa wanaendelea kujenga.
Antony Kisinga ambaye ni mmiliki wa majengo mbalimbali ya biashara eneo hilo amesema kitendo kinachofanywa na Kampuni ya Reli ni uonevu kutokana na kwamba miaka 10 iliyopota hajawahi kufuatwa na mtu yeyote kuhusiana na eneo hilo.
“Sasa napewa notisi ya kuvunja nyumba kwa siku 30 kwa mtu ambaye hajawahi kuninyooshea kidole wala hajawahi kuongea na mimi nilishtuka sana, hiki ni kitendo cha kibabe,”amesema Kisinga.
Hata hivyo alisema kuwa kutokana na kwamba ana nyaraka zote za umiliki wa eneo hilo na yeye sio mvamizi.
Kwa upande wake diwani wa kata hiyo, Charles Mkalakala amesema bomoabomoa hiyo imewaathiri watu wengi kutokana na eneo hilo kubadilishwa matumizi na Manispaa ya Moshi.
“Ni vizuri Serikali ikaangalia kuhusiana na zoezi hili kutokana na
kwamba kila mu ana hati miliki na kwamba hati ni mali ya Serikali, cha msingi Serikali iangalie kama walikubali kubadilisha matumizi basi wawaachie wananchi maeneo haya,”amesema Mkalakala.
Zoezi la bomoabomoa lilianza kutikisa Moshi baada ya Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli(Rahco), kutia timu mkoani hapa na kuvunja zaidi ya nyumba 500 .
Wananchi Wa Kilimanjaro Wahaha na Bomoabomoa Wamtaka Waziri Lukuvi Kuingilia Kati
0
September 16, 2017
Tags